TAKUKURU YACHUNGUZA MGOGO CHAMA CHA USHIRIKA UDURU NA MWEKEZAJI

 Na Gift Mongi

Hai


Mgogoro uliopo kati ya chama cha ushirika Cha Uduru kilichopo wilayani Hai na mwekezaji Makoa Farm ambaye amekodishiwa shamba lenye ukubwa wa ekari 368 umechukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, (TAKUKURU), mkoani Kilimanjaro kuingilia kati.


Hii inakuja baada ya kila upande yaani mwekezaji ambaye ni raia wa ujerumani, Elizabeth Stegimaya na uongozi wa chama hicho kufikisha malalamiko katika taasisi hiyo



Kwa mujibu wa mkuu wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro, Frida Wikes ni kuwa uongozi wa chama cha ushirika ulipeleka malalamiko ofisini kwake ukimtuhumu mwekezaji huyo kabadilisha matumizi ya ardhi kinyume cha sheria 


Alisema makubaliano yaliyokuwepo ni kuendeleza zao la kahawa lakini matumizi ya ardhi yamebadilishwa na kwa sasa anaendesha shughuli za utalii ambazo ni kinyume na makubaliano waliyokubalina lakini pia shughuli hizo hazitoi nafasi za ajira kama ambavyo ni dira ya ushirika huo.


Kwa upande wake mwekezaji huyo Elizabeth Stegimaya naye alipeleka malalamiko katika taasisi hiyo akilalamika kuingiliwa katika shughuli zake licha ya kuwa alifuata taratibu zote za ubadilishaji wa matumizi ya ardhi na kuwa vielelezo vyote anavyo na pia alishirikisha uongozi wa chama cha ushirika lengo lake hilo. 


Sifuel Mafuwe ni mwenyekiti wa chama cha ushirika Oduru ambapo alisema baada ya kuona matumizi ya ardhi yamebadilishwa waliamua kufuata taratibu zote ili kumuondoa mwekezaji huyo katika shamba lao hilo.


Alisema baraka walizipata kutoka kwa mrajisi wa vyama vya ushirika ambaye ndiye mlezi wa vyama hivyo ambapo alimtaka mwekezaji huyo kuondoka baada ya kuvunja mkataba waliowekeana na mwenye shamba.


Alisema tayari walishapata mwekezaji mwingine ambaye alikuwa tayari kujenga hoteli ya kitalii katika shamba hilo kwa makubaliano ya miaka 33 na baada ya hapo jengo hilo lingebaki mali ya wanaushirika.


Alisema uwekezaji huo ungechangia kwa kiwango kikubwa upatikanaji wa ajira kwa jamii inayowazunguka tofauti na ilivyo sasa ambapo hakuna fursa za ajira jambo ambalo ni kinyume na dira ya ushirika.



0 Comments:

Post a Comment