MAHAKAMA YAAMURU UPELELEZI KESI YA MAUAJI LOLIONDO KUHARAKISHWA



MAHAKAMA ya hakimu Mkazi Arusha imeuagiza upande wa jamhuri kuharakisha upelelezi wa kesi ya kula njama na mauaji ya askari polisi mwenye namba G 4200 Koplo Garlus Mwita inayokabili washitakiwa 24.

Aidha, mawakili wa utetezi wameiomba mahakama mwachie mshitakiwa wa 18, ambaye ni mama mwenye watoto watano akiwemo mdogo wa miaka miwili anayekosa haki ya kupata malezi ya mama kwani kwa sasa wanaangaliwa na baba pekee.

Amri hiyo ya mahakama imetolewa leo Agosti 5, 2022 na hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Herieth Mhenga wakati akitoa uamuzi mdogo kwenye shauri hilo la mauaji namba 11/2022.

"Upande wa mashitaka mnatakuwa mhakikishe upelelezi wa shauri hili unakamilika mapema ili washitakiwa wakasikilizwe na mahakama kuu," alisisitiza hakimu mkazi huyo.
Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesia akiteta jambo na wakili, Alute Mughway mara baada ya shauri hilo kuahishwa


Amesoma uamuzi mdogo huo mbele ya wakili wa serikali, Upendo Shemkole na mawakili wa utetezi wakiongozwa na Ally Mhyella, Jeremiah Mtobesya, William Ernest,  Salum Mwambo, Vean laizer, John Lairumbe, Jonas Masiaya na Paul Kisabo, Maria Mushi na Jebra Kambole.

Hakimu Mhenga amesema kuwa baada ya kupitia hoja za mawakili wa pande zote imeona pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi kutaka mahakama hiyo iendelee na taratibu za kusikiliza shitaka la kwanza la kula njama halina mashiko.

Alisema kuwa sheria ya uendeshaji wa mashauri ya jinai inaelekeza endapo mashitaka yamefanyika kwa kufuatana au kwa mlolongo yanapaswa kusikilizwa kwa pamoja.

Awali akirejea hoja za mawakili hao ambapo mara baada ya wakili wa serikali, Shemkole  aliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu upelelezi haujakamilika ambapo wakili wa utetezi, Peter Madeleka alipinga kuahirishwa kwa shauri hilo akidai kuwa kosa la kula njama liko ndani ya mamlaka ya mahakama ya hakimu mkazi na inaweza kulisikiliza na kulitolea uamuzI kosa la kwanza la kula njama ila  ikakubali mahakama kuahirisha kesi kwa kosa la mauaji.


Hakimu Mhenga aliendelea kueleza wakili Madeleka aliomba mahakama hiyo ipange tarehe ya kusikilizwa kwa kosa hilo la kula njama. 

Alisema hoja hiyo ilipingwa na wakili wa serikali, Shemkole kwa kike alichoeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo na makosa hayo yametendekea kwa mlolongo na hayawezi kutofautishwa hivyo akaomba maombi ya wakili Madeleka yatupwe.

"Mahahakama imezingatia hoja za pande zote mbili na kwa kuzingatia sheria ya uendeshaji mashauri ya jinai inasema makosa yaliyofanyika pamoja yanapaswa kusikilizwa kwa pamoja," alieleza hakimu Mhenga na kuongeza 

...Mahakama hii imeona haiwezekani kuyatenganisha makosa hayo ya kula njama ya kuua na kuua (akarejea kifungu cha sheria) kwa sababu makosa yanaweza kuwekwa pamoja kama yametokea kwenye mlolongo mmoja,"

"Nakubaliana na wakili Madeleka kuwa kosa la kula njama linaweza kusikilizwa na mahakama hii lakini kwa sababu kwangu limekuja kwenye hati ya mashitaka moja pamoja na kesi ya  mauaji ambayo mahakama hii haiwezi kuisikiliza nimeona haiwezekani kuyatenganisha makosa hayo,".


"Kama alivyoeleza kula njama si 'serious offence' na inaweza kusikilizwa na mahakama hii lakini kwa kuwa imewekwa pamoja na kosa la  mauaji hivyo mahakama hii haiwezi kuyatenganisha makosa haya na kusikiliza kosa la kula njama za kuua na likaacha hilo la mauaji ambalo mahakama hii haiwezi kusikiliza,".


Hivyo hakimu Mhenga alieleza kuwa mahakama hiyo inaendelea kukamilisha  jukumu lake la kisheria la kutaja kesi hiyo mpaka upelelezi utakapokamilika na kukiwa na ushahidi wa kutosha  washitakiwa hao watapelekwa mahakama kuu kwa ajili ya shauri hilo kusikilizwa. 


Baada ya uamuzi huo wakili wa utetezi, Mhyellah aliomba upande wa jamhuri utoe majibu juu ya maombi walitowasilisha juu washitakiwa wa 18,19 na 27 ambao ni wagonjwa na wanaendelea kuteseka gerezani.

Wakili wa utetezi Mushi alieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa wa 18 ni mama wa watoto watano ambapo mtoto mdogo ana miaka miwili hivyo anaomba aachiwe ili akawahudumie kwani kwa sasa wanahudumiwa na baba peke yao.


Mtuhumiwa namba 18, 19 na 27 upande wa mashitaka walisema walilipokea wakasema watatuletea majibu leo kwa sababu washitakiwa hao bado wanaendelea kutesema 

Mushi mshitakiwa namba 19 ugonjwa wa sukari anatakiwa kupata mlo maalum na siku ya jumapili hakuna mlo huo upande 



Hakimu Mhenga alisema upande wa jamhuri umesikia hoja hizo  hivyo wanaweza kukaa na viongozi wao wakaona umuhimu wa kuharakisha upelelezi ambapo shauri hilo limeahirishwa mpaka Agosti 17, 2022 litakaporudi kwa ajili ya kutajwa.


Washitakiwa kwenye shauri hilo ni pamoja na Molongo Paschal, Albert Selembo,  Lekayoko Parmwati, (21) Sapati Parmwati, (30) Ingoi Olkedenyi Kanjwel, (20) Sangau Morongeti,Morijoi Parmati, (20) Morongeti Meeki, Kambatai Lulu,(40) na  Moloimet Yohana,(37).

 

Wengine ni  Ndirango Senge Laizer, (52) Joel Clemes Lessonu, (54)  Simon Nairiam Orosikiria, (59)  Damian Rago Laiza, Mathew Eliakimu, (41) Luka Kursas, (49)  Taleng'o Twambei Leshoko, (37) Kijoolu Kakeya, (56)   Shengena Killel, (34) Kelvin Shaso Nairoti, (33) , Wilsom Tiuwa Kiling, (32), James Mumes Taki (28), Simon Saitoti, (41), na Joseph Lukumay



Awali Julai 14, mwaka huu Wakili wa Serikali Shemkole aliwasomea upya washitakiwa hao makosa yao ambapo alidai kuwa kuwa kosa la kwanza ni kula njama ya mauaji ambalo linawakabili  washitakiwa wote ambapo wanadaiwa katika tarehe na sehemu isiyofahamika walipanga njama ya kuua maafisa wa serikali na polisi  waliokuwa wakishiriki kuweka mipaka kwenye Pori Tengefu la Loliondo.


Katika shitaka la pili la mauaji wakili huyo wa serikali alidai  kuwa mnamo tarehe 10 Juni 2022 katika  eneo la Ololosokwan wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha kwa nia ovu washitakiwa hao walisababisha kifo cha askari polisi mwenye namba G 4200 Koplo Garnus Mwita.

Washitakiwa hao wamerejeshwa mahabusu kwenye gereza la mkoa la Kisongo kwani shauri la mauaji linalowakabili halina dhamana.





0 Comments:

Post a Comment