CHUO cha Taifa cha Utalii, (NTC) tawi la Arusha wameiomba ofisi ya Katibu Tawala mkoani Arusha, (RAS), Athuman Kihamia kuwasaidia kupata ardhi kwa ajili ya ujenzi wa mabweni kwenye eneo lililopakana na chuo hicho.
Ombi hilo limetolewa
leo Machi 25, 2022 na Mkuu wa chuo hicho Tawi la Arusha, Dkt Maswet
Masinda, wakati wa mahafali ya vijana wanagenzi 111 waliogharamiwa mafunzo
hayo na ofisi ya waziri mkuu ambapo mgeni alikuwa Katibu tawala huyo.
Amesema kuwa
tatizo kubwa linalowakabili ni ufinyu wa eneo huku akiainisha kuwa jirani yao
ambaye yupo kwenye hafla hiyo analo eneo
kubwa ambalo halijaendelezwa hivyo
akaiomba ofisi ya RAS ione namna inaweza kusaidia waweze kupata eneo dogo la
kujenga mabweni.
" Eneo kwa ajili
ya madarasa na ofisi tunalo, lakini mabweni yanatakiwa yawe mbali kidogo na
eneo la madarasa kwa hiyo mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa chuo cha Taifa
cha Utalii tunakuomba na tunaiomba ofisi yako kwa namna ya kipekee sana
itusaidie kupata eneo hilo," amesema Dkt Masinda na kuongeza.
... Serikali imepania
kuboresha na wadau wetu wa utalii wako tayari kutusaidia katika ujenzi wa
hosteli kwa ya ujenzi wa mabweni kwa ajili ya vijana
wetu,".
Dkt Masinda amesema
kuwa Wizara iliwapangia wanachuo 120 lakini waliohitimu lel ni 111
ambapo wengine waliacha masomo kutokana changamoto mbalimbali lzilizowakabili
ambazo si za kifedha kwa sababu walikuwa wanasoma bure.
"Wengine walipata
kazi, waliajiriwa wakiwa masomoni wakapima wakaamua kuendelea na kazi badala ya
kuendelea na mafunzo," amefafanua Dkt Masinda.
Amesema kuwa hayo ni
mafunzo kwa awamu ya tatu ambapo kwa NTC ni awamu ya kwanza kuwapokea jumla ya wanafunzi
140 ambapo kampasi ya Arusha wamepokea wanafunzi 120 na 120 wengine
walipokelewa kwenye kampasi yao ya Bustani.
"Sasa tunaenda awamu
ya pili, pia wizara imepanga kuongeza idadi, nitoe wito kwa vijana waweze
kuzitumia hizi fursa.Wakati nafasi zilipotolewa kampasi ya Arusha ilipokea
maombi 1,103 kati yao walichaguliwa ni 120," amesema Dr Masinda na
kuongeza
"Tunaweza tukaona
ni jinsi gani hitaji lilivyokuwa kubwa kwa Taifa kwamba vijana wanahitaji
kusoma. Vijana wetu tunawaasa pale mnapopata fursa mzitumie vizuri kwani
kuna wengi wanaohitaji kupata fursa hizo lakini wanazikosa,",
Kwa upande wake Katibu
tawala mkoa wa Arusha, Kihamia akiongea na wahitimu hao amewaasa kuwa mafunzo
waliyopatiwa kwa miezi hii sita ikiwemo miwili katika mafunzo kwa vitendo
anaamini wameshabobea kilichobaki ni wao kwenda kufanya kazi na kuwa waadilifu
na waaminifu huku wakitumia weledi waliopewa hapo chuoni kwa kulitumikia Taifa .
"Mimi niwaombe
vijana wangu ambao mmehitimu hapa leo na ambao hawapo hapa, muwekee mkazo sana
uzalendo wa nchi yetu na uaminifu na uadilifu kwa sababu itasaidia kurahisisha
utekelezaji wa mipango ya serikali," amesema Kihamia na kuongeza.
...Unaweza kuajiri
vijana kadhaa baada ya muda unakuta tuhuma huyu kaiba hiki huyu kafanya hiki,
huyu kamtukana bosi wake huyu kaenda kinyume na maadili yake.
...Kizazi cha miaka ya
sasa kuanzia 35 kurudi chini kwa kweli…. Ila naamini licha ya mafunzo mliyopata
ya utalii na ukarimu
naamini wamewaandaa tabia zetu zikae vizuri.
…Ili kuona kwamba
hamfanyi yale mambo ambayo ni kinyume na maadili na kwa jinsi mnavyopendeza na
kung'ara naamini na weledi tabia na mienendo yenu inang'ara,”.
Wanachuo waliohitimu
chuoni hapo waliwashukuru Ofisi ya
Waziri Mkuu iliyogharamia mafunzo yao, mkuu wa Chuo, wakufunzi kwa kuwafundisha na RAS kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali yao.
" Shukrani zetu
za dhati na z kipekee ziende ofisi ya Waziri Mkuu kwa ufadhili huu wa mafunzo
kwa asilimia 100 kwa vijana wa Kitanzania bila ubaguzi wowote,” alisema
mwanachuo huyo akisoma risala ya wahitimu na kuongeza.
“Kwa kipitia mafunzo
haya kuna wenzetu wamenufaika kwa kupata ajira mara baada ya kumaliza mafunzo
yao ya vitendo kwenye mahoteli na migahawa mikubwa jijini Arusha,”.
Kwa upande wake
mhitimu, Fadhila Kitundu amesema kuwa anashukuru kupata mafunzo hayo anayoamini
yamemfanya awe bora zaidi na mwenye kuweza kuhimili ushindani wa soko la ajira.
“ Naamini mimi
ninasifa zote zinazohitajika na tabia yangu ni njema na itaonekana kwa jamii na
wataweza kunitofautisha na vijana wengine,” amesisitiza Kitundu.
Kwa upande wake
mhitimu mwingine, Lilian Lameck amesema anajisikia vizuri na furaha kwa sababuaimeweza kupata ajira
kupitia kozi hiyo.
“Nawakaribisha vijana
wengine waje chuo cha utalii kampasi ya ya Arusha lakini pia
wanaweza kwenda Mwanza au Dar es Salaam zilipo kampasi mbili,” amesisitiza
Lilian.
Naye Lussa Melembuke
ameishukuru ofisi ya waziri mkuu kwa kuwaambini lakini pia wakufunzi wa chuo
cha Taifa cha utalii, Arusha kwa kuwaamini kwani haikuwa rahisi kupenya kwenye
kundi la vijana zaidi ya 1000 waliokuwa wakiwania nafasi hizi 120
“Tunaahidi tutaendelea
kupambana kutimiza ndoto zetu lengo ni kujiajiri au kiajiriwa Taifa liendelee
kinufaika na uwepo wetu.” Smediditixs Melembuke.
Agosti
mwaka jana Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa alinukuliwa akisema Tanzania nzima kuna
vijana takribani 45,000 ambao wamesambazwa katika vyuo vyote vya Serikali na
vya binafsi ambapo watapatiwa mafunzo ya ufundi stadi kwa miezi sita kwa
kugharamiwa na serikali.




0 Comments:
Post a Comment