WEUSI KUKIWASHA COCORIKO KIJENGE EID MOSI

 




Kundi la wanamuziki wa Hiphop la Weusi litakiwasha jijini Arusha siku ya Eid Mosi kwenye ukumbi wa Cocoriko Kijenge.


 Mkurugenzi wa Cocoriko Club, John Mdenye, amewaeleza waandishi wa habari leo kuwa tayari maandalizi yamekamilika. 

"Kesho tutakuwa na shoo kubwa, kundi zima la Weusi watakuwa hapa. Shoo hii tumeiandaa vizuri kweli na wasanii wote wa Arusha watakuwa hapa,"

"Tutakuwa na wasanii wengine wa bendi yetu kama Michael Jackson na wengine hivyo nawakaribisha wananchi wote wa Arusha wanaopenda burudani waje kusherekea sikukuu za Eid.,"

"Kuanzia mchana tutakuwa na burudani mbalimbali, tutakuwa na chakula na vinywaji waje wale wanywe wafurahi pamoja na familia zao,". 

Mdenye amesema kiingilio wakati wa usiku kitakuwa shilingi 10,000 kwa eneo la kawaida na  VIP wameandaa vizuri kwa watu special watalipa 15,000  kwa hiyo akawakaribisha sana wapenda birudani, wote kufika na kupata burudani.
  
"Shoo hii haijawahi kufanyika sehemu yoyote hapa Arusha. Kama mnavyojua Weusi ni watoto wetu wa huku Arushahivyo shoo hiii tumeiandaa kwa staili kitofauti ambayo wateja wetu na wapenzi wa Weusi watafurahia shoo hii," amesema.


Shabiki wa Weusi, Kolumba Mbabaz amesema kuwa Weusi wameamua kuiheshimisha Arusha kwani kwa sasa wana albam yao ya Air Weusi ambapo hii ni shoo yao ya kwanza jijini hapa tokea waachie albam hiyo.

"Arusha sasa ni halisi kutokana na hali ya hewa ya baridi na mvua za hapa na pale hivyo Weusi tumewapa jukumu moja siku ya Eid Mosi yaani wafanye shoo watu wajisahau  kama wako kwenye Arusha ya baridi," amesema Kolumba.

Amesema nyimbo za weusi zinaweza kusikilizwa na watu wa rika zote kwani zimezingatia maadili hivyo wazazi wanaweza kufika wa watoto wao Cocoriko na wakaondoka wakiwa wamesuuzika roho zao kutokana na burudani watakazopatiwa

 

Kundi la Hiphop la Weusi linaundwa na Joh Makini, Lord Eyez, Nikki Wapili na Gnako Werawera ambapo wana zaidi ya miaka mitatu tokea wafanye shoo jijini hapa.



Wasanii hao ambao ni wenyeji wa Arusha wanaoendesha shughuli zao za kumuziki jijini Dar es Salaam hivi karibuni wameachia rasmi albamu yao  mpya kwa jina 'Air Weusi'.

Ina nyimbo 14 na mbili tu ndiyo za ambapo walioshirokishwa ni Khadoja Kopa na Big Boso J.O.J. O.



0 Comments:

Post a Comment