DK. SHOO AONGOZA MAZISHI YA MAMA MAEDA




MKUU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini,(KKKT) , Askofu, Dk Fredrick Shoo ameongoza ibada ya mazishi ya mmliki wa hotel ya kitalii ya Golden Rose, Caroline Hanna Maeda, (87) aliyefariki Mei 3, mwaka huu kwa shinikizo la damu.

Aidha katika ibada hiyo oliyohudhuriwa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji la Arusha na maeneo mengine ya nchi  iliyofanyika leo KKKT, Usharika wa  mjini Kati, Askofu Dk Shoo, ameshirikiana na Askofu wa KKKT, Daiyosisi ya Kaskazini Kati, Dk Solomon Massangwa na mch Sinyatt Laizer 



Marehemu, Mama Maeda ni mtoto wa tatu wa Mangi David Mlanga Mareale ambapo ameacha watoto sita wajukuu 14 na vitukuu nane.


 Dk Shoo ambaye pia ni askofu wa KKKT Daiyososi ya Kaskazini ametoa pole kwa familia na wafiwa wote, na kusema hakuna wakati tunachoka kuishi na mtu kwa sababu maisha yake yanagusa watu wengine hivyo akadai njia pekee ya kumuenzi ni kuishi maisha ya kutumikia Mungu na kuwasaidia wengine

"Bila kimung'unya maneno, mama Maeda amegusa maisha ya wengi hivyo tumeondokewa na mtu muhimu. Mama Maeda ameondoka ameacha alama kwenye jamii,  kanisani, serikali na hata katika maisha ya mtu mmoja mmoja tungependa kumuomba Mungu amuache lakini mipango ya Mungu ni tofauti na mipango ya wanadamu," amesema Dk Shoo.

Amesema kuwa marehemu mama Maeda alikuwa na imani kubwa ndiyo sababu hata mume wake kufariki aliweza kusonga mbele.

"Kwenye zaburi ya 90 tunamuomba Mungu atupatie moyo wa hekima. Usikimbie matatizo kabiliana nayo kwa imani.
Wengine wakiwa wajane ni kulia kuweka mikono kichwani na kwenda kuombaomba. Simama imara Yesu yupo atakufanikisha," amesema Dk Shoo na kuongeza.

"Mama Maeda aliendelea kusimama imara kwenye kazi ya Mungu kwa kusaidia jirani, yatima, wajane awepo mtu anasema asante Mungu kwa mtu huyu bila kusahahu kazi ya Mungu.

Alikuwa anajali sana maendeleo ya familia yake, mara ya mwisho nilipoongea naye alinishirikisha juu ya namna familia kushirikiana


"Maisha tunayoishi hapa duniani yana mwisho, kifo  cha mama Maeda kitukumbushe maisha ya hapa duniani yana mwisho hata hapa kuna atakayefuata japo hatujui ni nani," amesema askofu Dk Shoo.

WAJANE JIFUNZENI UJASIRI KUPITIA MAISHA YA MAMA MAEDA

Askofu Dk Massangwa amesema wajane wajifunze ujasiri kwa mama Maeda kwani baada ya mume wake kufariki akimuachia watoto sita wakiwa na umri  wadogo hakukata tamaa alisonga mbele na kusimamia biashara yao ya mabasi ya NBS.

"Hata ulipotokea msukosuko wa kiuchumi aliamua kuingia kwenye biashara ya hoteli ya kitalii za Golden Rose pamoja na Arusha View," amesema Askofu Dk Masangwa na kuongeza .

"Caroline Hanna Maeda alipenda kanisa, alihudumia kanisa, alimpenda Mungu ambaye kanisa ni mali yake.
Imani ya Kristo si ya kukimbia bali ya kukumbatia kwani inatuhakikishia kuna maisha baada ya maisha haya hapa duniani,".

Mbali na hoteli hizo marehemu mama Maeda, aliendeleza biashara za malori, mashamba makubwa ya kilimo na kituo cha mafuta cha BP Market Square.


1Wakorinto 15:50-55 

SHUGHULI ZA KIJAMII NA KIIMANI ALIZOSHIRIKI MAREHEMU 

Marehemu, mama Maeda enzi ya uhai wake  alikuwa mzee wa Usharika KKKT Mjini Kati, mwanzilishi na mfadhili Mkuu wa Kwaya ya Uinjilishaji KKKT Mjini Kati, Mjumbe wa Halmashauti Kuu Jimbo la Arusha Mashariki, mfadhili mkuu wa vituo vya watoto yatima kikiwemo kile cha Good Samaritan Orphanage, Moshono.

Marehemu Caroline Maeda alikuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa bodi wa shule ya sekondari Weruweru pamoja na Maasai girls ya Monduli.

Aidha atakumbukwa kwa namna alivyosaidia watoto wengi walioshindwa kusomeshwa na familia zao kuanzia shule ya msingi mpaka vyuo vikuu.

Rotary Club walimpatia tuzo kwa kutambuamchango wake katika kujitoa na kuisadia jamii, mshauri mzuri kwa wajane na wenye shida mbalimbali.

ALICHANGIA UHURU WA TANZANIA, KENYA NA ZIMBAWE

Marehemu Mama Maeda alisaidia harakati za uhuru wa mataifa ya Tanzania, Kenya na Zimbabwe kwa kuwahifadhi Mwalimu Julius Nyerere na Jommo Kenyatta wa Kenya.

"Pia alisaidia ukombozi wa nchi ya Zimbabwe kwa kuwahifadhi na kuwafadhili familia ya Alex Chitepo alikuwa mpigania uhuru Zimbabwe,".

SALAMU ZA RAMBIRAMBI  


Watu na taasisi mbalimbali walitoa salamu za rambirambi akiwemo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya TFA, Peter Sirikwa aliyesema TFA wamesema wamepoteza kiongozi na mshauri alikuwa nao begabega nyakati zote.

Chama cha Wanasheria Wanawake, TAWLA ambapo mtoto wa marehemu, Martha anafanya kazi huko.

Chama cha Wamiliki wa hoteli za daraja la kati wamlilia Caroline Hannah Maeda wanakumbuka na kuenzi mchango wake katika kukuza sekta hiyo.

Mwanafunzi wa marehemu mama Maeda, Dk Ngowi aliyesema alifundishwa na mama Maeda mwaka 1953 kwenye shule ya Mamba Kotela . 

"Alitufundisha kwa upendo na wengi aliotufundisha tulipata nafasi kubwa serikalini na alikuwa akitukumbuka vizuri wanafunzi wake mara ya mwisho alinionyesha picha aliyopiga pamoja na sisi wanafunzi wake wakagi akitufundisha Mamba Kotela,  " anasema Dk Ngowi.


Naye Mchungaji  John Njau  amesema kuwa mwaka 
2001 mpaka 2003 nilikuwa mchungaji kwenye  usharika wa KIA.

"Niliwashirikisha Walter pamoja na mama Maeda juu ya uhitaji wa kanisa na walitusaidia sana hivyo alikuwa anashiriki kwenye ujenzi wa kazi za Mungu," amesema mchungaji Njau.





0 Comments:

Post a Comment