SHULE 13 ARUSHA WASAINI KUPATIWA MAZIWA

Kaimu Msajili bodi ya maziwa Tanzania ,Noely Byamungu akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kusaini makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa unywaji wa maziwa shuleni , pembeni yake ni Mkurugenzi wa kampuni ya maziwa ya Kilimanjaro Fresh ,Irfhan Virji.


SHULE  13 za msingi mkoani Arusha zimetia sahini  na Bodi ya maziwa Tanzania ya makubaliano ya utekelezaji wa mpango wa  unywaji wa maziwa shuleni .


Akizungumza katika hafla fupi ya kusaini makubaliano hayo, Kaimu  msajili Bodi ya maziwa nchini, Noely Bya Mungu  amesema kuwa lengo la mpango huo Ni kutekeleza maagizo yaliyotolewa na serikali na kwa Arusha mpango huo  ulianza January 14, mwaka huu .


Byamungu, amesema kuwa mpango huo kwa Sasa umeanza kwa majaribio kwa kuzihusisha shule 13 za msingi za Serikali (9)na binafsi (4)zenye zaidi ya wanafunzi 10,000 ambapo watatekeleza mpango huo kwa miezi 12


Byamungu alisema kuwa shule zilizochaguliwa kuanza mpango huo wa unywaji maziwa,shuleni hizo zinatoka katika Halmashauri za wilaya za Arusha Jiji (8)Arumeru(2) na Longido 3



Mkurugenzi wa kampuni ya maziwa ya Kilimanjaro Fresh ya jijini Arusha, Irfhan Virji ambao ndio watekelezaji wa mradi huo alisema kwamba malengo yao ni kuboresha afya za watanzania na kusaidia kukuza soko la uzalishaji wa maziwa nchini.


Virji,alisema kwamba mbali na kusambaza huduma ya maziwa mashuleni pia wanataraji kuweka friji mbalimbali za maziwa yao katika ofisi za serikali pamoja na mabenki kama njia mojawapo ya kutanua huduma wanayozalisha.


Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi, amesema kuwa mipango huo ni fursa kwa wafugaji na wenye viwanda vya maziwa kujiongezea kiapato na kukuza Uchumi wa viwanda Nchini


Lyamongi amesema kuwa mpango huo umelenga kuwajengea watoto utamaduni wa kunywa maziwa, ili baadae kuwe na kizazi ambacho kutakuwa kinatumia maziwa na bidhaa zake, Kama sehemu ya maisha yao yao ya kila siku na kujenga Afya ya Akili na mwili.


Naye Mwanasheria kutoka bodi ya maziwa Tanzania, Edwin Bantulaki, amesema kuwa Bodi ya maziwa nchini ndiyo chombo kikuu Cha kudimamia Tasnia ya Maziwa nchini hivyo imeamua kuingia makubaliano na kiwanda Cha Galax Food Beverages LTD kuuza maziwa shuleni


Amesema kuwa malipo hiyo muuzaji atalipwa na kamati ya shule,atakuwa na jukumu la kupeleka maziwa shuleni pia atalipwa punde atakapokabidhi maziwa au atakapokabidhi maziwa awamu nyingine.


Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa shule waliopo kwenye mradi huo mwalimu Mwl.Mkuu wa shule ya msingi Longido Charles Efatha Mbando amesema kuwa wameupokea kwa mikono miwili,na kuwashirikisha wazazi kwa kutambua kuwa maziwa ni sehemu ya mlo kamili kwa watoto.


Mbando amesema kuwa kutokana na mpango wa unywaji maziwa kwa wanafunzi mashuleni ,wanatarajia kwa mwaka 2021 idadi ya ufaulu kwa wanafunzi itakuwa juu kwani maziwa yanajenga Afya uelewa wa wanafunzi mashuleni .

Aidha mpango huu Mkoani Arusha ulianza tarehe 14 Januari 2021 ,wakati timu ya Bodi ya maziwa iliookutana na wataalam kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa Afisa (Mifugo,Afisa Elimu,Afisa Ustawi wa Jamii na Afisa Lishe )na wadau wa Elimu .Wazazi ,wakuu wa shule na kamati ya Chakula ya Shule)

Imeandikwa Na Happy Lazaro,Arusha



0 Comments:

Post a Comment