MADAKTARI bingwa wawili wa hospitali ya St Thomas ya jijini Arusha waliofariki mapema wiki hii wanatarajiwa kuzikwa wiki ijayo kwa nyakati tofauti .
B Marangu mkoani Kilimanjaro na Njombe.
Madaktari hao ambao vifo vyao vimeacha simanzi jijini Arusha ni daktari bingwa na upasuaji,Dk Lamweli Henry Makando, ambaye ni mmoja wa wamiliki wa hospitali ya St Thomas anayetarajiwa kuzikwa Marangu mkoani Kilimanjaro.
Mwingine ni daktari bingwa wa magonjwa ya watoto, Dk Simon Kavavila alifariki Jumatatu anayetarajiwa kuzikwa Njombe.
Madaktari hao walifariki kwa nyakati tofauti ambapo mmoja alifariki jumatatu na mwingine Jumanne, baada ya kulazwa katika hospitali ya St Thomas na baadaye kukimbizwa hospitali ya KCMC.
Mmoja wa wamiliki wa hospitali ya St Thomas,
Dk Julius Msuya leo Machi 6, amesema kuwa Dk Makando anatarajiwa kuzikwa Jumatatu Machi 8, 2021 Marangu na Dk Kavavila atazikwa Njombe.
Kabla kukumbwa na kifo madaktari hapo, walikuwa wamelazwa pamoja katika hospitali ya St Thomas, akianza kuumwa Dk Kavavila na baadae Dk Makando.
Madaktari hao wameacha pigo kubwa mkoani hapa hasa kutokana na huduma za kitabibu walizokuwa wakitoa kwa muda mrefu na kwa umahiri mkubwa.
Mmoja wa wananchi, Rose Mollel anasema yeye aliwahi kumpeleka mtoto wake kutibiwa na Dk Kavavila ambapo aliweza kumpatia dawa lililosaidia kumaliza kabisa shida ya mwanaye ambaye alikuwa tayari ameshazunguka naye hospitali kadhaa bila mafanikio.
Mwananchi mwingine, Lucy Ngowi, anasema kuwa amekuwa akijifungua kwa kufanyiwa upasuaji ambapo ana watoto watatu na mara zote ni Dk Makando ndiye alimfanyia upasuaji hivyo anasema kifo cha Dk huyo kimemuumiza yeye pamoja na familia yake.
".
Mgaga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Dk Widson Sichalwe alisema vifo vya madaktari hao vimesikitisha sana
0 Comments:
Post a Comment