MAKAZI YA MASISTA YAVAMIWA WAIBIWA FEDHA NA VIFAA

 


MASISTA wa shirika la Franciscan wamevamiwa kwenye makazi yao na kituo cha malezi ya vijana kisha kuibiwa fedha zaidi ya shilingi milioni 16 na kuharibiwa vibaya samani na vifaa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 6.


Waliovamia ni kundi la watu zaidi ya 40  wanaodaiwa kutoka kampuni ya udalali ya First World Investment court ambapo walikuwa wamebeba nondo walizotumia kuvunja makofuli ya lango kuu la kuingia kwenye makazi hayo na mengine ya ndani.


Tukio hilo lililotokea jumatano iliyopita (januari 13, 2021) majira ya saa 7:45 mchana kwenye makazi yao yaliyopo mtaa wa engosingiu, kata ya Sinoni, jijini Arusha na kutolewa taarifa kwenye kituo cha polisi Muriet iliyosajiliwa namba MTR/RB/186/2021.


Uvamizi huo ulizua taharuki kwa masista hao pamoja na majirani zao kutokana na namna watu hao walivyokuwa wakitumia nguvu kuvunja makofuli ya milango kwa kutumia nondo na majembe kisha kutoa vitu nje.



Akiongea na waandishi wa habari sista kiongozi, Meseret Melese  alisema kuwa fedha zilizoibwa zilikuwa zimetolewa benki kwa ajili ya kwenda kutekeleza shughuli za shirika hilo kwenye mikoa mbalimbali ambapo kutokana na tukio hilo imewalazimu kufuta safari zote.



Alisema kuwa watu hao waliiba kompyuta mpakato moja huku wakiharibu kumpyuta ya mezani, friji na kuvunja samani mbalimbali wakati walipotumia nguvu kurusha nje vitu hivyo.


Alisema kwenye makao hayo ya masista na malezi ya vijana na kazi za kichungaji  yanatumiwa na masista 10 pamoja na vijana nane anaoandaliwa kuwa masista ambapo wakati watu hao wakivamia walikuwa masista sita na vijana nane
Sista Mesele alisema kuwa siku ya tukio akiwa ndani alisikia kelele ambapo alipotoka nje alimuona mlinzi wa getini akimfuata akiwa anakimbia akimwambia kuna watu wengi wanalazimisha kuingia ndani.


Alisema kabla hajamaliza kumweleza tayari watu hao walikuwa wameshafika alipokuwa hivyo wakawa wanaelekea ndani ambapo alijaribu kuongea nao lakini hawakumsikiliza.


Sista Mesele alisema kuwa mtu mmoja alimweleza kuwa wamekuja wanawataka waondoke kwenye eneo hilo kwani tayari siku 14 walizopaswa kuwa wameondoka kama walivyoamriwa na mahakama zimekwisha.


" Niliwaambia tayari tumeweka zuio mahakamani kwani eneo letu halijaahinishwa kwenye amri ya mahakama waliyotuletea . Hawakutaka kunisikia walikimbia wakaingia ndani wakaanza kibeba vitu wanatupa nje," alisema sista Mesele na kuongeza.



Mnaona hivi vitu vyote vitanda, magodoro, samani kompyuta tumevikusanya hapa, tulivirudisha ndani baada ya mvua kunyesha  lakini vyote vilitupwa nje.



Walikimbia baada ya gari la polisi kufika hapa na kuwataka waonyeshe hiyo amri ya mahakama inahowapa uhalaki wa kutoa vitu.

 Hapo walijitokeza Hamad Omary na dada mmoja alikuwa ameongozana naye na mtu mwingine aliyesema yeye ni dalali lakini wengine wote walipanda kwenye gari waliyokuwa wamekuja nayo wakakimbia,".


Kamanda wa polisi mkoani hapa, Salum Hamduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa mpaka sasa watu saba wanashukiliwa ingawa hakutaja majina yao.
Tayari mkuu wa wilaya ya Arusha, Kenani Kihongosi aligika kwenye makazi hayo ya masista ambapo aliagiza jeshi la polisi kuwakamata wale wote waliohusika na tukio hil.


0 Comments:

Post a Comment