HUYU HAPA BILIONEA MWENYE UMRI MDOGO ZAIDI DUNIANI

  


Kylie Jenner

Kylie Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea ya gazeti la Forbes.

Kylie ambaye ndiye mdogo zaidi katika familia ya Kardashian amepata utajiri wake kutokana na biashara ya vipodozi.

Akiwa na umri wa miaka 21-alianzisha na anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka mitatu sasa na kuingiza mapato ya takriban dola milioni $360m mwaka jana.

"Sikutarajia chochote. Sikujua hali ya baadae.Lakini kutambuliwa inafurahisha. Ni jambo zuri la kunitia moyo," Bi Jenner aliliambia jarida la Forbes.

Alifikia mafanikio haya mapema kuliko muasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg ambaye alikuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.





1 comment: