ALIYEDAI MTOTO WA LOWASSA MIKONONI MWA POLISI


Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema wanamshikilia Fatuma Chikawe kwa tuhuma za kudanganya kuwa ni mtoto wa Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa.

Anakamatwa ikiwa imepita wiki moja tokea Fatuma kujitokeza kwenye vyombo vya habari na kudai ametelekezwa na baba yake ambaye ni Lowassa.

Aliyasema hayo  kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, aliyekuwa aliendesha zoezi la kusikiliza malalamiko ya wanawake waliotelekezewa watoto na wanaume ambapo alisisitiza wahusika watoe taarifa za ukweli

0 Comments:

Post a Comment