Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Abdul Nondo ambae pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliyedaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha usiku wa Machi 6, mwaka huu jijini Dar es Salaam amepatikana Mafinga mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Juma Bwire amethibitisha kupatikana kwa Nondo Machi 7, mwaka huu ingawa hakuwa tayari kueleza Kwa kina juu ya tukio hilo kwa kile alichofafanua kuwa mwanafunzi huyo bado anaandika maelezo kwenye kituo cha Mafinga.
Nondo kabla ya kutekwa alimtumia rafiki yake ujumbe mfupi kupitia simu ya kiganjani uliosomeka “I AM AT HIGH RISK” ambapo baada ya hapo alipotafutwa kupitia simu zake ziliita tu kabla ya hazijazimwa kabisa.
Mkurugenzi wa idara ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Paul Kisabo alisema “Nondo amepatikana yupo mafinga kituo cha polisi muda huu. Amezinduka jioni ya leo akiwa ametupwa, akauliza watu kwamba yuko wapi wakamwambia yupo mafinga. Akajivuta kwenda kituo cha polisi,” .
“Bahati nzuri alikuwa anakumbuka namba moja tu ya dada yake akaomba simu polisi na kumpigia dada yake, Dada yake pia akamjulisha baba yake mdogo wa huku dar tuliyekuwa nae leo," alifanya Kisabo na kuongeza.
“Then kupitia namba ya polisi kituo cha polisi Mafinga Nondo ameongea na baba yake mdogo tuliyekuwa nae leo kupitia simu ya afande. Amenyang’anywa laini zake za simu ila simu yake anayo. Ila yupo salama.”
Source Milardayo.com

0 Comments:
Post a Comment