MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, (AfCHPR), leo inatarajia kutoa uamuzi kwenye rufaa iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe, Johnson Nguza (Papii Kocha) wakipinga ya adhabu waliyohukumiwa mwaka 2004 ya kutumikia kifungo cha maisha gerezani.
Uamuzi huo wa shauri hilo namba 006/2015 unatolewa wakati tayari wanamuziki hao raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa huru baada ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais, John Magufuli, Desemba 9, mwaka uliopita.
Uamuzi huo wa shauri hilo namba 006/2015 unatolewa wakati tayari wanamuziki hao raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa huru baada ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais, John Magufuli, Desemba 9, mwaka uliopita.
Awali uamuzi huo ulikuwa utolewe juzi lakini Rais wa AfCHPR, Jaji Sylvaine Ore kutoka nchini Ivory Cost, alilazimika kuahiridha mpaka leo kwa kile alichoeleza kuwa upande wa waleta maombi hawakufika mahakamani hapo.
Hata hivyo baadhi ya wanasheria wameielezea hatua hiyo kuwa inaweza kuwasafisha wanamuziki hao kutokana na makosa waliyotiwa hatiani endapo itakubali maombi yao ya kuwafutita makosa kwani Rais Magufuli aliwapa msamaha wa adhabu lakini kumbukumbu iliyopo inaonyesha ni kweli walibaka na kulawiti watoto 10 wenye umri kati ya miaka sita na nane.
"Kesho ndiyo naweza kutoa maoni kisheria kwani uamuzi utakuwa umetoka, ila nachoweza kusema Rais alitoa msamaha wa adhabu ya kifungo cha maisha kwa kina Nguza lakini hakufuta makosa waliyotiwa hatiani kuwa walibaka na kulawiti hii bado iko kwenye rekodi za mahakama na kokote watakapoulizwa waliwahi kutiwa hatiani itabidi waandike hivyo," alisema wakili mmoja ambaye hakuwa tayari jina lake liandikwe gazetini.
Hata hivyo alisema hana uhakika kama mahakama hiyo ina nguvu za kisheria ya kusikiliza na kufanyia uamuzi maombi ya kuna Nguza.
Awali katika maombi yao ya msingi Babu Seya na Papii Kocha waliiomba Mahakama ya Afrika kutoa uamuzi kuwa haki zao zilivunjwa hivyo wanaomba waachiwe huru na kulipwa fidia.
Pia waliomba wawezeshwe kupata msaada wa sheria huku wakiitaka Mahakama hiyo iteue wataalamu watakaotoa ufafanuzi wa hoja za kesi yao na kuisaidia kufikia wajibu wake.
Waliendelea kudai kuwa mwenendo wa shauri lao haukufanyika kwa kuzingatia haki na hati ya mashtaka dhidi yao ilikosewa kuandikwa tarehe ambayo tuhuma za makosa yao zilidaiwa kufanywa hivyo wakashindwa kutayarisha utetezi wao.
Walidai kuwa mahakama iliyowatia hatiani ilijielekeza katika ushahidi wa upande wa mashtaka pekee usioshirikisha ushahidi mwingine na Serikali ya Tanzania kupitia maofisa wake, ilivunja misingi ya haki za binadamu na sheria za kimataifa.
Wanamuziki hao maarufu hapa nchini walidai kuwa baada ya kukamatwa hawakuelezwa mapema kuhusu mashtaka waliyokuwa wakituhumiwa nayo na waliwekwa chini ya ulinzi kwa siku nne bila kuwa na mawasiliano na kupata fursa ya kuonana na mwanasheria au mtu mwingine ye yote.
Walidai wakiwa chini ya ulinzi, polisi waliwatesa na kuwatukana na baadaye ofisa mmoja wa polisi aliwaeleza kuwa wanatuhumiwa kwa ubakaji.
KESI YA AWALI
Nguza na wanawae watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa kituo cha Polisi cha Magomeni Dar es Salaam na baadaye walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16 mwaka 2003.
Watuhumiwa hao pamoja na mwingine aliyejulikana kwa jina la Mwalimu walishtakiwa kwa tuhuma 10 za ubakaji na 11 ya kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka sita na nane. Watuhumiwa wote walikana mashitaka yao.
Baada ya kusikilizwa kesi hiyo, Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam ilitoa hukumu Juni 25, mwaka 2004 ambapo Iliwatia hatiani kwa kifungo cha maisha jela huku mtuhumiwa wa tano, Mwalimu akiachiwa huru.
Nguza na wanawe walikata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania Oktoba 30, 2013 ambako wafungwa wawili Francis Nguza na Nguza Mbango walishinda rufaa yao.
Wanadai kwamba mashtaka dhidi yao yalitungwa na hivyo hukumu iliyotolewa haikujikita katika ushahidi wenye nguvu katika sheria.
0 Comments:
Post a Comment