Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM (UV CCM) Taifa iliyokutana kwa dharura mchana huu chini ya Mwenyekiti wao, Kheir Denis Jemes imetengua uteuzi wa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM Taifa Jokate mMwengelo kuanzia leo
Taarifa hiyo iliyotolewa kupitia mtandao wa twitter wa UVCCM imesema kuwa Jokate Mwegelo ametenguliwa katika nafasi hiyo ambapo amehudumu katika nafasi hiyo kwa takribani miezi 11 toka amelipoteuliwa April 2017.
Kikao hicho kilichomtengua Jokate kimefanyika katika ukumbi wa secretariet White house Mjini Dodoma.
Katibu Mkuu wa UV CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema sababu za kutenguliwa kwa Jokate inatokana na uamuzi wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja huo iliyokutana kwa dharura leo mchana chini ya Mwenyekiti wake, Kheri.
Amesema kikao hicho kiliazimia kwa pamoja kumuondoa Jokate kwenye nafasi hiyo huku akidai hatua hiyo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya baraza hilo ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa ni ajenda ya kikao.
“Itoshe tu kusema ni utaratibu wa kawaida ndani ya CCM pamoja na jumuiya zake kufanya mabadiliko ya aina yoyote pale wanapoona inafaa,” amesisitiza Shaka.

0 Comments:
Post a Comment