Diwani wa kata ya Themi Mh Melance Kinabo amekagua Eneo Mtaro wa kupitisha maji katika eneo la mtaa wa Corridor Kwenye kata ya Themi.
Ujenzi wa Mtaro huo wa maji uliochukua Muda mrefu kukamilika ulizua Hali ya kutokuwa na maelewano baina ya Mkandarasi aliyepewa Tenda hilo wa PPF na Wananchi.
Mzozo huo ulitokana na Hali ya Kutokamilika kwa ujenzi kuwa wakati na kupelekea barabara kutopitika nyakati za mvua kwa kuwa na matope na Vumbi Kali wakati wa jua Kali.
Diwani Kinabo amesema Amekuwa akipokea malalamiko Mengi toka kwa wakazi wa Corridor Kwenye kata yake hivyo kufuatilia suala hilo kwa ukaribu.
Ingawa Jitihada zetu za Kumpata Mkandarasi huyo zinaendelea kwa sasa Ujenzi wa Mtaro huo tayari uanendelea na unatarajiwa kukamilika mapema pasipo kuchukua kipindi kirefu.




0 Comments:
Post a Comment