AJALI: GARI LA MAJI YA KILIMANJARO LAGONGANA NA NOAH WANNE WAFARIKI


WATU wanne wanadhaniwa kufa huku wanne wengine wakinusurika baada ya  gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongana uso kwa uso na gari la kampuni ya vinywaji baridi ya Bonite bottlers ya Mjini Moshi.


Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa tisa alasiri eneo la Kikafu wilayani Hai ambapo majina ya waliojeruhiwa na kufariki hayajapatikana mara moja.

Mashuhuda wa ajali hiyo wanadai kuwa chanzo ni gari kubwa la vinywaji baridi lenye namba za Usajili T 835 DJR kuamua kuyapita magari yaliyokuwa mbele hivyo kikutana uso kwa uso na Noah iliyokuwa ikitokea Moshi Mjini kuelekea Sanya Juu wilayani Siha.

Gari hilo ambalo lilikuwa na trela lenye  T  974 BTA ambalo ubavuni lina nembo ya maji ya Kilimanjaro huku kioo cha mbele kukiwa na nembo ya coca cola.


Tutaendelea kuwahabarisha zaidi




0 Comments:

Post a Comment