Hii Picha haihusiani na tukio la hapa chini ila tumekuwekea kwa uhusiano wa kinachozungumziwa. Picha kutoka Maktaba Google. |
Wizara ya Afya ,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na watoto imetoa taarifa ya kuifungia kwa wakati taasisi isiyoya kiserikali Shirika la Community Health Education Services and Advocacy (CHESA) .
Kulingana na Taarifa hiyo Shirika hilo limefungiwa kwa sababu za kuhusianishwa na Sakata la ndoa ya Jinsia moja ambapo inasemekana Shirika hilo la kijamii inatuhumiwa kuratibu warsha kuhusu masuala ya Jinsia moja tarehe 17 October 2017 katika hoteli ya Peacock jijini Dar Es Salaam.
Aidha Taarifa hiyo imeelekeza kuwa uongozi wa Shirika hilo kusitisha shughuli zake zote ikiwa pamoja na kufunga ofisi zake zote ili kupisha uchunguzi.
Copy ya Taarifa hiyo hii hapa chini
0 Comments:
Post a Comment