BREAKING NEWS: Baada ya Golugwa Leo kaitwa TAKUKURU Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha

Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Elias Mungure ameitwa TAKUKURU kwa mahojiano.

Hapo Jana Taasisi hiyo huru inayoshughulika na kupambana na kuzuia rushwa ilimuita Mwenyekiti na kiongozi wa kikanda wa chama hicho kikubwa cha upinzani Amani Golugwa.

Duru za Habari zimedai kuwa Viongozi hao wanahojiwa kufuatia sakata la Madai ya kununuliwa madiwani wa chama hicho  ambapo mbunge kupitia Chama hicho Joshua Nasari wa Arumeru Mashariki aliwasilisha ushahidi kwa taasisi ya ya Kupambana na Rushwa Tanzania TAKUKURU kuwa madiwani hao walinunuliwa kwa rushwa na wateule wa Rais.

0 Comments:

Post a Comment