BREAKING: Alichosema Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Arusha Baada ya kuhojiwa TAKUKURU kwa saa zaidi ya Tatu.



Mapema hii leo tulikuripotia kuwa katibu wa CHADEMA mkoa wa Arusha Elias Mungure aliitwa TAKUKURU kwa ajili ya mahojiano.

Huu ni mwendelezpo wa Taasisi hiyo huru nchini Tanzania kuendelea kuwahoji viongozi mbaliombali juu ya sakata la madai ya kurubuniwa kwa madiwani wa CHADEMA, mahojiano haya yanakuja mara baada ya Mbunge Joshua Nasari kuwasilisha ushahidi kuwa madiwani wao walinunuliwa na si kwamba walikihama chama hicho kwa ajili ya kumuunga mkono Rais wa Tanzania John Magufuli kama walivyodai Madiwani waliojiuzulu.

TAKUKURU jana ilimuhoji Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Arusha Mh. Amani Golugwa 

VOA TV News & Habaritanzaniagracemacha.com  haikuwa mbali kukujuza hili.. Muda huu tumempata Katibu huyo akitoka hapa TAKUKURU baada ya mahojiano ya zaidi ya saa tatu.


Mh. Mungure anasema "Nataka kuwaeleza wananchi wa Arusha kuwa Takukuru wanafanya kazi .. tunataka taasisi zingine zifanye kazi kama Takukuru, sisi tumekuewa Transparent kwa serikali yetu tunataka uwazi kwenye shughuli zetu."
Aidha Mungure ameeleza kuwa Takukuru kama taasisi ya Serikali inafanya kazi kwa  weledi hivyo wananchi wawe na subira.

Video ya VOA TV News hii hapa play kusikia FULL INTERVIEW.


0 Comments:

Post a Comment