AY, Mwana FA na Mkito watangaza kuja na Label ya Kimataifa

Rapa Mwana FA pamoja AY wameungana na kampuni ya Mkito.Com kuanzisha record label itayokuwa ikifanya kazi chini yao pamoja na uongozi waliouteuliwa.

FA ameiambia Bongo5 kuwa wamefikia makubaliano hayo baada ya kuoana nchini Tanzania hakuna label za muziki zinazofanya kazi kwa viwango vya kimataifa.
“Sisi na Mkito tumeamua kuanzisha ushirikiano partnership, Mimi na AY tulikaa chini tukaona hakuna record label ambayo inafanya kazi kama zinavyotakiwa. Kwahiyo sisi tumeona kama hii ni fursa kwa sababu wao wanavitu ambavyo tunavikosa na sisi kuna vitu ambavyo wanavikosa ndio maana tukaamua kuonganisha nguvu kuangalia namna ambavyo tunaweza kwenda mbele,” alisema FA

0 Comments:

Post a Comment