Klabu ya Singida United imefanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza wa Ligi kuu dhidi ya watukutu kutoka Mwanza, klabu ya Mbao FC.

Singida United wamepata goli lao la kwanza kipindi cha kwanza goli ambalo halikudumu kwani baadae kunako dakika ya 35 Mbao FC wakachomoa na hadi mapumziko matokeo yaklikuwa 1-1.
Goli la ushindi la Singida United lilifungwa kunako kipindi cha pili cha mchezo huo na hadi dakika 90 zinamalizika, Singida United 2 Mbao FC 1.
0 Comments:
Post a Comment