HABARI: Mungure aongoza wananchi kufanya usafi

DIWANI wa  Kata ya Kikatiti, Elisa  Mungure, (CHADEMA), ameongoza zoezi la Usafi kwenye vijiji vya  Nasholi na Kikatiti.

Zoezi hilo ambalo lilipata mwitiko mkubwa kutoka kwa wanakijiji  lilianza majira ya saa 12 Asubuhi na kumalizika  saa 6 mchana.

Diwani Mungure alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi juu ya masuala mbalimbali ya Maendeleo kwenye kata hiyo hasa uboreshaji wa miundombinu ya barabara, elimu, afya na uwezeshaji wa vikundi vya vijana na wanawake.
Aidha aliwaomba wazidi kuomuombea mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, apone mapema kwani kwa Sasa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Agha Khan jiji Nairobi nchini Kenya baada ya watu wasiofahamika kumshambuliwa kwa kupiga risasi zaidi ya 30 akiwa ndani ya gari wakati akiingia nyumbani kwake mjini Dodoma majira ya mchana.
Huo ni utaratibu waliojiwekea viongozi wa Kata, vijiji na wananchi wa kufanya usafi kwenye maeneo yao kila mwisho wa wiki ambapo hutumia kauli mbiu
'Mji safi,Chama safi'.
 
"CHADEMA tunaweza, MUNGU MPONYE TUNDU ANTIPAS LISU. Tanzania inamtegemea, tunampenda, tunamwamini, ni kiongozi pekee amejitokeza kupinga ukandamizaji wa demokrasia waziwazi ," alisisitiza Mungure.








0 Comments:

Post a Comment