Marekani imesema imefanikiwa katika jaribio lake la kurusha kombora la kudungua la mfumo wa hali ya juu wa kukabiliana na makombora-THAAD.
Idara ya Ulinzi wa Makombora ya Marekani imetoa tangazo hilo jana Jumanne. Idara hiyo imesema mfumo wa kuzuia makombora uliopo Kodiak, Alaska, uligundua, kuufuatilia na kudungua kombora la masafa ya kati linalolengwa na mfumo huo.
Ilisema kombora hilo lililorushwa angani kutokea kwenye ndege ya kijeshi ya kubebea mizigo juu ya anga la Bahari ya Pasifiki kaskazini mwa Hawaii.
Hili ni jaribio la kwanza tangu mfumo wa THAAD ulipopelekwa nchini Korea Kusini kuanzia mwezi April mwaka huu kama jibizo kufuatia Korea Kaskazini kuongeza tishio la makombora. Hapo awali jaribio hilo lilipangwa kufanyika kabla ya Korea Kaskazini haijatangaza kuwa ilifanya jaribio la kombora linaloweza kuvuka mabara mapema mwezi huu.
Idara hiyo imesisitiza mafanikio kwenye jaribio hilo, ikisema limeimarisha uwezo wa kujilinda wa Marekani dhidi ya tishio la makombora la Korea Kaskazini

0 Comments:
Post a Comment