Korea Kaskazini imetangaza kupitia shirika la habari linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo kuwa imefanikiwa kurusha kombora lingine la masafa ya kati ililolipa jina la "Polar Star Two".
Taarifa hiyo ilitolewa kwenye majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi ya leo Jumatatu kwa saa za Japani. Taarifa hiyo ilisema Kiongozi Mkuu wa nchi hiyo Kim Jong Un alisimamia zoezi hilo.
Shirika hilo la habari linalomilikiwa na serikali lilisema Kim alipongeza urushaji huo wa kombora na kusema ulikuwa na mafanikio ya asilimia 100 na kwamba aliridhia jaribio hilo.
Jeshi la Korea Kusini limesema kombora hilo liliruka umbali wa kilomita 560 kutoka usawa wa bahari na kuanguka kwenye Bahari ya Japani zaidi ya kilomita 500 kutoka kwenye eneo liliporushwa.
0 Comments:
Post a Comment