TAARIFA MUHIMU: Masikitiko ya Mbunge Godless Lema kufuatia kunyimwa nafasi ya Kutoa salamu za pole na rambi rambi katika Maombolezo ya kuaga miili ya Wanafunzi wetu wa Lucky Vincent , Maombolezo yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheigh Amri Abeid jijini Arusha.

Ikumbukwe kuwa ajali hiyo ilitokea 6/5/2017  ambapo moja ya gari la shule ya Lucky Vincent ilipata ajali wakati ikielekea Eilayani Karatu kwa ajili ya mtihani wa joint. Nakupelekea kupata ajali maeneo ya milima ya Rotia , ajali iliyoondoka na maisha ya ndugu zetu zaidi ya 30.
  Tunamnukuu Mh. Godless Lema 
"Leo katika msiba wa kuaga Wanafunzi waliofariki katika  ajali . Mimi kama Mbunge mwenyeji niliyefiwa Jimboni kwangu pamoja na Mayor tulihudhuria maombolezo hayo, ilikuwa ni itifaki ya kawaida kabisa kuelewa kuwa Mbunge pamoja na Mayor watapaswa kutoa salamu za rambi rambi au kuwashukuru wageni waliofika kwa ajili ya kutupa pole .

Nilisikia toka jana jioni kuwa katika maombolezo haya leo kuwa Viongozi wa Chadema watapaswa kutokuongea , nilimpigia simu Mbunge wa Ngorongoro Mh Ole Nasha , nikamweleza ubaguzi mchafu unavyopangwa katika jambo hili muhimu la kuaga watoto wetu, alinihakikishia kuwa Makamu wa Rais hasingeweza kukubaliana na ujinga huu.

Kwenye ratiba nilipoingia uwanjani , jina langu lilikuwepo kwenye ratiba kwa ajili ya salamu za rambi rambi, lakini baada ya Mkuu wa Mkoa kukabidhiwa itifaki, mambo yalibadilika nailionekana dhairi kuwa sitakiwi kabisa kutoa pole kwa watu wa jimbo langu waliofikwa na msiba huu mbaya. M/kiti Mbowe aliandika meseji kwenda kwa M/ Rais kukumbusha umuhimu wa wenyeji kutoa salamu , Makamu wa Rais baada ya kupokea meseji hiyo , alimwita Mkuu wa Mkoa , ndipo ilionekana kama kuna ushindani unatokea kati yao , lakini hatukuweza kabisa kupata nafasi ya kutoa salamu kwa wapendwa wetu.

Wabunge wa ccm waliokuwepo ambao ni mawaziri wote waliweza kutoa pole ,huu ni ubaguzi uliojaa ujinga na chuki mbaya kisiasa , nitauleza madhara yame kwenye hotuba yangu kesho , lakini nafikiri watoto wanafuata walichofundishwa na wazazi ,pengine ingekuwa ni usaliti Mbunge Lema kusalimia na kuwapa pole watu wake mbele ya Makamu wa Rais . Ni wazi sasa kwamba tofauti yetu sisi kama Nchi na Syria ni wakati.

Nawashukuru wote waliotukimbilia kwa matatizo yaliyotokea Arusha , Mungu awabariki sana. Msiogope , Mungu adhiakiwi apandacho Mtu ndicho avunacho" Mbunge wa Arusha Mjini Mh. Godless Lema

0 Comments:

Post a Comment