HIVI PUNDE: 19 Wauawa shambulio la Manchester 50 Majeruhi

Polisi katika mji wa Manchester nchini Uingereza wanasema watu 19 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kwenye mulipuko uliotokea ndani ya ukumbi wa tamasha la muziki.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametaja tukio hili kama kitendo cha ugaidi.
Ikiwa itathibitishwa kuwa ni shambulio la kigaidi, litakua mbaya zaidi kuwahi kukumba Uingereza tangu Julai mwaka 2005 wakati zaidi ya watu 50 walikufa kwenye misery Ru ya milipuko  London.
Watu walioshuhudia mulipuko huo wa Manchester wamesema mwamziki wa Marekani Ariana Grande alikua amemaliza kuwatumbuiza mashabiki wake, wakati mulipuko mkubwa ulisikika na kutikisa ukumbi mzima.

Mashahidi wamesema kuona misumari iliyotapakaa sakafuni na harufu ya vilipuzi.

0 Comments:

Post a Comment