VIDEO UPDATES : Ni pigo lingine ACT-Wazalendo Wakili Msando ajiuzulu

Mh. Zitto Kabwe (Kushoto) Na Wakili Albert G. Msando

Mshauri wa chama cha ACT -
Wazalendo Wakili Albert G Msando  ameandika barua ya kujiuzulu wadhifa wake huo.

Kiongozi mkuu wa ACT- Wazalendo Mh. Zitto Kabwe Amesema amepokea rasmi barua ya kiongozi huyo mshauri wa chama.

Zitto amempongeza Bw. Msando kuwa kiongozi bora wakati wote alipokuwa akiitumikia chama kwa nafasi mbalimbali.

"Nimepokea barua ya Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu cha ACT Wazalendo.

Ndugu Msando anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu  "kuishi Kama mfano Kwa jamii inayonizunguka".

Ndugu Albert Msando amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama mwanachama.

Nikiwa Kiongozi wa Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.

Ndugu Msando Alberto ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika mitihani iliyomkumba." Zitto Kabwe

0 Comments:

Post a Comment