Exclusive: Millioni 18 za rambi rambi bado zinashikiliwa na Polisi


Mapema leo Saa 9:30 Am waliripoti kituo kikuu cha polisi (Central Police) Arusha Meya wa jiji la Arusha Mh. Kalisti Lazaro , Katibu wa TAMONGSCO Kanda ya kaskazini Mh. Leonard Mao, mkuu wa shule ya Lucky Vincent ,na viongozi wengine kwa lengo la Kukabidhiwa fedha kiasi cha 18 Millioni ambayo ilikuwa rambi rambi kwa ajili ya ajali ya Lucky Vincent au kutajwa kesi inayowakabili viongozi hao na kufikishwa mahakamani viongozi hao endapo wangebainika na kosa.

Mapema kabla ya 9:30 Am Habari Tanzania Grace Macha ilikuwa jirani na kituo kikuu cha polisi ili kibaini kama zoezi hilo linafanyika , Punde aliwasili Katibu wa TAMONGSCO Bw. Leonard Mao ambapo alidai kumuona kaimu kamanda wa polisi "Nimeshafika mapema hapa nimeonana na kaimu kamanda ameniambia tufike tena ijumaa"

Kuhusu Fedha za rambi rambi
"Fedha zipo kwa OCD pamoja na simu yangu"  Bw. Mao

Sawia na hilo Blogu hii ikamtafuta Meya Kalisti Lazaro kwa njia ya Simu ambapo alisema "Niwasili central nikaambiwa ineahirishwa kwa hiyo turipoti ijumaa" Kalisti Lazaro

Akizungumza kuhusu fedha hizo pamoja na tukio nzima la kukamatwa viongozi hao pamoja na Waandishi wa habri Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha RPC Mkumbo alisema "Bado sijui chochote kuhusu hizo fedha pamoja hatua zinazoendelea dhidi ya viongozi hao akiwemo Meya"


0 Comments:

Post a Comment