CHINA : Updatesy:, Msimamo wa China Upo Imara kuondoa Nyukilia kwenye rasi ya Korea Kaskazini,


Geng Shuang 


China imetupilia mbali ukosoaji wa Korea Kaskazini kuwa nchi hiyo imeungana na Marekani katika kuweka shinikizo kwa Korea Kaskazini juu ya mipango yake ya nyuklia na makombora.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Geng Shuang jana Alhamisi wakati akizungumza na waandishi wa habari aliukanusha ukosoaji huo uliotolewa juzi Jumatano na chombo cha habari kinachomilikiwa na Korea Kaskazini.

Geng alisema msimamo wa China wa katika kuondoa silaha za nyuklia kwenye Rasi ya Korea uko wazi na hauyumbiyumbi na vivyo hivyo msimamo wake wa kuendeleza ujirani mwema na mahusiano mazuri ya kirafiki na Korea Kaskazini.

Aliongeza kuwa kwa miaka mingi China imekuwa ikichambua na kukabiliana na masuala ya msingi kulingana na manufaa yake bila upendeleo na kwa usawa.

Gazeti la Chama cha Kikomunist cha China, gazeti la People's Daily na gazeti lingine linalohusiana na chama cha siasa la Global Times hivi karibuni yametoa maoni ya kukosoa mipango ya nyuklia na makombora ya Korea Kaskazini. Ukosolewaji wa Korea Kaskazini ulikuwa wa moja kwa moja katika magazeti hayo ya China. 

Gazeti la Global Times lilitoa tahriri nyingine katika chapisho lake lililotoka jana Alhamisi asubuhi. Lilisema Korea Kaskazini inajiingiza katika aina fulani ya uhasama juu ya mpango wake wa nyuklia.

0 Comments:

Post a Comment