Waziri Makamba aeleza mkakati a serikali kuhusu Ruaha mkuu

Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais-muungano na mazingira January Makamba mapema leo aliongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya uharibifu a mazingira hususani katika bonde la mto Ruaha mkuu mkoani Iringa.
Mh. January Makamba
Mpango huo ambao makamu wa Rais na mawaziri watano wataelekea Iringa siku ya Jumanne ya April 11 2017 lengo likiwa ni kukagua na kuangalia bonde la mto Ruaha ambalo linakabiliwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hususani wa ardhi.
Uharibifu wa mazingira katika bonde la mto Ruaha kwa kiasi kikubwa unatokana na shughuli za kibinadamu zisizo endelevu zinazofanywa katika maeneo ya vyanzo vya maji pamoja na vilele vya milima, miteremko ya milima na katika mabonde.
Baada ya kugundua uharibifu huo unaoendelea kufanyika katika bonde la mto Ruaha, serikali kwa kushirikiana na wadau imeona kuna haja ya kuwa na mtazamo mpya wa namna ya kukabiliana na changamoto za mto Ruaha Mkuu kwa ufanisi zaidi.

0 Comments:

Post a Comment