POLISI ARUSHA WANASA MIRUNGI

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TAARIFA YA KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WATANO WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA BHANGI MAGUNIA SABA (7).
MNAMO TAREHE 01/08/2014 MUDA WA SAA 3:30 USIKU HUKO KATIKA MAENEO YA SANAWARI JIJINI ARUSHA, ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIPATA TAARIFA TOKA KWA RAIA WEMA ZILIZOELEZA KUWEPO KWA WATU AMBAO WALIKUWA WANASAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA AINA YA BHANGI.
MARA BAADA YA TAARIFA HIYO, ASKARI HAO WALIFUATILIA NA KUFANIKIWA KUWAPATA WATUHUMIWA WAWILI AMBAO NI HUSSEIN S/O RASHID (35) MKAZI WA SAKINA NA NDIO DEREVA WA GARI HILO PAMOJA NA SEBASTIAN S/O WILBERT MAHONDE (37) FUNDI MAGARI MKAZI WA ILBORU WALIOKUWA WANATUMIA GARI AINA YA TOYOTA COROLLA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 589 AZS LILILOKUWA LINATOKEA EKENYWA NGARAMTONI KUELEKEA NCHINI KENYA KUPITIA NJIA YA TARAKEA.
ASKARI HAO WALIENDELEA NA UPEKUZI NA KUBAINI GUNIA TANO ZA MADAWA HAYO NDANI YA GARI HILO ZENYE UZITO WA KG 171. KATIKA MAHOJIANO WATUHUMIWA HAO WALIKIRI KOSA HILO NA KUELEZA KWAMBA MADAWA HAYO WALIUZIWA NA MTU AITWAYE FLORA W/O JOHN (38) MKULIMA MKAZI WA EKENYWA.
ASKARI HAO WALIENDELEA KUFUATILIA TAARIFA HIZO AMBAPO LEO TAREHE 05/08/2014 WALIKWENDA ENEO LA EKENYWA-NGARAMTONI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MUUZAJI FLORA W/O JOHN PAMOJA NA MUME WAKE AITWAYE JOHN S/O MELEJI (45) MLINZI WA TPRI MKAZI WA EKENYWA AMBAPO MARA BAADA YA UPEKUZI WALIKUTA GUNIA JINGINE LA MADAWA HAYO AINA YA BHANGI.
MBALI NA WATUHUMIWA HAO PIA ASKARI HAO WALIMKAMATA LOSERIANI S/O METELAMI (21) MKULIMA MKAZI WA EKENYWA AKIWA NA GUNIA MOJA LA MADAWA HAYO AMBAYE ANAISHI JIRANI NA WATUHUMIWA WENZAKE HIVYO KUFANYA JUMLA YA GUNIA ZILIZOKAMATWA KUWA 7 (SABA).
MPAKA HIVI SASA TUNAENDELEA KUWAHOJI WATUHUMIWA WOTE WATANO NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI PINDI UPELELEZI UTAKAPOKAMILIKA.  ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI,
(SACP) LIBERATUS SABAS          TAREHE 05/08/2014.