CHAMA Cha Demokrasia na
Maendeleo, (CHADEMA) kimesema kuwa mbinu mbalimbali zinazofanywa na watawala ikiwemo kuwajeruhi na kuwauwa viongozi na wanachama
wao kwa mabomu na silaha za moto kwa lengo la kurududisha nyuma harakati zao za kuwaamsha
wananchi kujua haki zao na kuzidai haitafanikiwa.
Hayo yalisemwa juzi na Mwenyekiti
wa chama hicho wilayani Arusha, Ephata Nanyaro wakati alipokuwa akitoa msaada
kwa wahanga wa matukio ya mabomu yanayodaiwa kurushwa na polisi kwenye mikutano
mbalimbali ya chama hicho.
Alisema kuwa mbinu hizo ovu
haiwezi kufanikiwa kwa kuwa Chadema wanamtegemea Mungu hivyo wataendelea
kushinda jambo alilodai kuwa hata sasa licha ya matukio mengi ambayo wananchi
wameuwawa na kuumizwa lakini bado wameshikamana na harakati zinaendelea.
Nanyaro ambaye pia ni diwani wa
kata ya Levelos alisema kuwa wataendelea kupigania uhuru wa kweli wa Taifa hili
kwa lengo la kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao, kodi inayokusanywa
inatumika vizuri na nchi inaongozwa kwa misingi ya utawala bora huku uwazi
kwenye kila jambo ikiwemo mikataba mikubwa inayohusu rasilimali za umma
ikiwekwa wazi kwa wananchi.
“Msingi wa mauaji haya
yanayofanywa na vyombo vya dola ni kurudisha nyuma harakati zetu za kupigania
wanyonge na kuwaamsha watu kudai haki zao, wanatumia risasi tulizonunua kwa
fedha zetu wenyewe kwa kodi tunazolipa,
badala ya kutulinda wanatuua lakini sisi tunawaambia haya wanayoyafanya
hatukatishi tama bali yanatuongezea ari ya kupigania kuhakikisha nchi hii
inaongozwa kwa misingi ya utawala bora.” alisema Nanyaro.
Kwa upande wake Katibu wa chama
hicho wilayani hapa, Martin Sarungi alisema kuwa jumla ya wahanga 40 watapatiwa
vitu mbalimbali vilivyotolewa na wanachama na wapenzi wa chama hicho ikiwemo
fedha taslim, Sabuni, unga, mchele, matunda na vyakula mbalimbali.
Alisema kuwa kati ya wahanga hao 39 ni kutoka jiji la Arusha huku
mmoja akitokea wilayani Arumeru ambapo ni mjane wa aliyekuwa Mwenyekiti wa
chama hicho kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo aliyefariki kwa kukatwa na kitu
chenye ncha kali shingoni.
Wahanga hao ambao ni wale
walipoteza ndugu zao, waliumizwa maeneo mbalimbali ya mwili na hivyo kupata
ulemavu wa kudumu siku ya maandamano na mkutano wa chama hicho wa janiari 5,
2011 ambapo polisi waliwauwa kwa risasi watu watatu Juma Ismail, Denis Shirima
na mmoja wa Kenya huku wananchi wengine kadhaa kujeruhiwa.
Wahanga wengine ni wale wa tukio
la June 15, mwaka jana ambapo bomu ambalo Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,
Freeman Mbowe alidai lilirushwa na polisi kwenye viwanja vya Soweto wakati
akifunga mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata nne za
Arusha ambapo walifariki watu watano akiwemo Katibu wa Chadema Kata ya Sokon1, Judith Mollel ambapo wengine kadhaa walijeruhiwa.
Aidha wahanga wengine ni wale
waliojeruhiwa Juni 18, mwaka jana wakati walipokusanyika kwenye viwanja vya Soweto
kwa lengo la kuagaa miili ya wenzao waliuwawa June 15 ambapo polisi
waliwatawanya wananchi hao bila kutoa taarifa ya onyo ya kuwataka kutawanyika
ambapo viongozi kadhaa wa chama hicho walikamatwa na kufikishwa polisi lakini
hakuna mashtaka yoyote yaliyofunguliwa dhidi yao.
DKT. LAZARO BUNUNGU ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA PERAMIHO
-
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimbo la Peramiho kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Dkt. Lazaro Komba Bunungu, amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya
kugo...
7 hours ago
0 Comments:
Post a Comment