MAUAJI mengine ya kutisha yametokea wilayani Arumeru baada ya mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 25 na 30 ambaye hajatambuliwa jina lake kukutwa amekufa huku mwili wake ukiwa umenyofolewa sehemu za siri na mikono yote miwili.
Kamanda wa polisi mkoani Arusha , Liberatus Sabas alisema kuwa mwili huo ulikutwa umetelekezwa katika mto Nambala wilayani Arumeru Mei 26, mwaka huu ambapo mpaka sasa imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali ya mkoa ya Mount Meru ukichunguzwa na madaktari .
“Mwili huo uligunduliwa na mashuhuda waliokuwa wanapita katika eneo hilo ndipo walipotoa tarifa kwa jeshi la polisi mkoani hapa, badhi ya askari walienda eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa na suruale aina ya “Jeans” iliyoshushwa hadi chini ya magoti huku baadhi ya viungo vyake vikiwa vimenyofolewa” alisema kamanda huyo wa polisi.
Kamanda Sabasi alisema kuwa wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha kifo hicho.
Wilaya ya Arumeru ilikumbwa na mauaji ya kutisha mwishoni mwa mwezi Aprili ambapo maiti za wanaume wanne zilikutwa zimetelekezwa kwenye maeneo tofauti zikiwa zimenyongwa shingoni kwa minyororo na nyingine kwa kamba ambapo wiki moja baadaye Mwenyekiti wa kata ua Usa River wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Msafiri Mbwambo aliuawa kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali.
0 Comments:
Post a Comment