Rais wa AfDB Amaliza Ziara ya Siku 4 Tanzania, Atunukiwa Shahada ya Heshima na UDSM πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸŽ“

 


Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Akinwumi Adesina, amekamilisha ziara yake ya siku nne nchini Tanzania (Juni 12–15, 2025) kufuatia mwaliko rasmi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akiwa nchini, Dkt. Adesina ametembelea miradi mikubwa inayofadhiliwa na AfDB ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato na barabara ya mzunguko ya Dodoma, akisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika miundombinu kwa maendeleo ya Afrika.



Juni 13, 2025, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilimtunuku Shahada ya Heshima ya Falsafa katika Sayansi kutambua mchango wake mkubwa katika maendeleo ya bara la Afrika kwenye sekta za miundombinu, kilimo, afya, nishati na mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Adesina aliondoka nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akieleza dhamira ya kuendeleza ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na AfDB kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.

0 Comments:

Post a Comment