Thursday, January 9, 2025

Mtoto Azaliwa Katika Boti ya Wahamiaji Akielekea Visiwa vya Canary

 


Mtoto wa kiume amezaliwa katika boti ya wahamiaji iliyosafiri kutoka Afrika hadi Visiwa vya Canary, na kuonyesha hadithi ya matumaini na changamoto za wahamiaji. 


Boti hiyo ilionekana kwa mara ya kwanza tarehe 6 Januari, karibu na kisiwa cha Lanzarote, wakati Uhispania ikisherehekea sherehe za Epifania.


Walinzi wa pwani walifika haraka baada ya mtoto kuzaliwa, wakikuta mama na mtoto, ambao walikimbizwa hospitalini kwa huduma za ziada. Nahodha wa boti ya uokoaji, Domingo Trujillo, alielezea kuwa walijua kuhusu mjamzito lakini waliguswa walipokutana na mtoto aliyezaliwa dakika chache zilizopita.


Kamanda wa helikopta alielezea kuwa kuzaliwa kwa mtoto ilikuwa “zawadi bora zaidi” waliyopokea siku hiyo, ambayo ilikua ni muhimu na ya kipekee. 

Safari kutoka Afrika hadi Visiwa vya Canary ni hatari sana, ambapo mwaka jana wahamiaji zaidi ya 46,800 walifanya safari hii ndefu na yenye changamoto kubwa.

No comments:

Post a Comment