Happy Lazaro,Arusha .
Hospitali ya Gemsa Polyclinic iliyopo mkoani Arusha imeanzisha kambi ya siku tatu ya upimaji na utoaji elimu wa saratani ya matiti na tezi dume bure Arusha wananchi wa mkoa wa Arusha kuanzia oktoba 24 hadi 26 .
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye kambi hiyo,Daktari wa magonjwa yote kutoka hospitali hiyo,Dokta Kelvin Kimal amesema kuwa , huduma hizo zote zinatolewa bure lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya saratani ya matiti na tezi dume kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kwani bado ni changamoto.
Dokta Kimal amesema kuwa, upimaji huo unaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa wananchi hao juu ya magonjwa hayo na kuweza kupata elimu namna ya kuzigundua dalili mapema kwani bado elimu ni changamoto.
Aidha Dokta Kimal amefafanua kuwa, changamoto iliyopo ni wananchi wengi kufika kupata matibabu ya magonjwa hayo hali ikiwa imekuwa mbaya zaidi jambo ambalo linakuwa ni changamoto katika kupata matibabu ,hivyo kupitia kambi hiyo wanaweza kupatiwa elimu namna ya kuzijua dalili mapema na kuweza kuwahi kupata huduma kabla tatizo halijawa kubwa zaidi.
"Tumeamua kuweka kambi hii kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na kuweza kupatiwa vipimo vya awali na kuweza kupatiwa elimu namna ya kuweza kujipima wenyewe pia "amesema .
Aidha amefafanua zaidi kuwa,vipimo hivyo vinapimwa kwa kutumia kifaa cha ultra sound na kuweza kuonana na madaktari na kuweza kushauriwa namna ya kufanya endapo watagundua kuwepo kwa dalili hizo .
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa hiyo ya huduma bure na matibabu kwani kutokea ni mara chache sana .
Kwa upande wake ,Daktari wa magonjwa yote ,Amne Munir Saggaf amesema kuwa, kambi kama hiyo walishafanya miaka miwili iliyopita ambapo mwitikio ulikuwa mkubwa sana wa wananchi ambapo wanatamani waifanye kila mwaka kwani uhitaji ni mkubwa sana .
Saggaf amefafanua kuwa,wamejitahidi kuboresha huduma hizo kwa mwaka huu lengo likiwa ni kuona wananchi wengi wa Arusha wanapata huduma hiyo na kuweza kupata matibabu pia.
"Katika kambi hii ya siku tatu tunatarajia kufikia wananchi Mia tano ambao tunatarajia watakuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao kwa kutoa elimu ambayo tutakuwa tumewapatia ili waweze kuzijua dalili za magonjwa hayo na kuweza kupata matibabu mapema. "amesema dokta Saggaf.
Mmoja wa wananchi waliopata huduma hospitali hapo,Januari Chami kutoka Sombetini amesema kuwa amefurahia huduma hiyo kwani unapata fursa ya kupata elimu kuhusu magonjwa hayo na dalili zake ili kuweza kuwahi matibabu mapema .
"Kwa kweli nimefurahi sana nimeweza kupima tezi dume na figo na nimekutwa sina shida yoyote nawaomba wananchi wa Arusha wajitokeze kwa wingi kuchangamkia fursa hii inayotolewa bure hapa hospitali ya Gemsa kwani ni adimu sana kupatikani .
0 Comments:
Post a Comment