Katika sherehe za miaka 47 ya CCM, Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini ongoza upandaji wa miti

Katika sherehe za miaka 47 ya CCM, Mwenyekiti wa UVCCM Moshi Vijijini, aongoza upandaji wa miti Kirua Vunjo Kusini, akisisitiza umuhimu wa kujali mazingira na kuenzi historia ya chama.




Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenail Shirima, leo ameongoza maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Sherehe hizo zilifanyika eneo la Kirua Vunjo Kusini, ambapo Mwenyekiti huyo alipanda mti kama ishara ya kujali mazingira na kuendeleza kampeni za upandaji miti. Hafla hiyo ilihudhuriwa na wajumbe wa UVCCM na wanachama wa CCM wakiungana kusherehekea mafanikio na historia ya chama hicho kikongwe. (Imeandikwa na Gift Mongi)

0 Comments:

Post a Comment