WANASHERIA WAKUMBUSHWA KUTOJITENGA NA JAMII

 


JAJI Mfawidhi mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Joachim Tiganga amewashauri wanasheria kutumia lugha nyepesi inayoeleweka kwa wananchi katika kutoa elimu badala ya kutumia misamiati migumu inayowafanya wananchi kushindwa kuelewa mpaka wahitaji mtu wa kuwatafsiria.


Ameyasema hayo leo, Februari mosi, 2023 wakati wa kilele cha wiki ya sheria ambayo kauli mbiu ya mwaka huu ni "Umuhimu wa utatuzi ww migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu :wajibu wa mahakama na wadau".


"Wananchi wanatuona sisi wanasheria ambao tunaitana wasomi kuwa tunajitenga nao hata kama jambo linaweza kujadilika kwa lugha nyepesi lakini sisi tunatumia misamiati migumu ya kitaaluma ambayo si rahisi kwa wao kuielewa," alisema Jaji Tuganga.

Hata hivyo aliwashukuru wasemaji kwenye hafla hiyo kwa kutumia lugha ambayo haikujumuisha misamiati migumu hata rejea walizofanya walitumia mifano ya kesi ili wale waliohitajika kupata ujumbe huo waliuoata ukiwa kamili bika kuhitaji tafsiri toka kwa watu wengi.


Akizungumzia faida za kumaliza migogoro kwa njia ya usuluhishi jaji Tiganga alisema kuwa inaweza kurejesha mahusiano ya kirafiki na kindoa, maafikiano kwenye migogoro ya kibiashara ambapo watu walioingia makubliano ya kimkataba wanafika mahali wanazungumza na kufikia makubaliano kwenye yale maeneo ambayo walikuwa wakitofautiana.

"Upatanishi ambao unakuwa katika mashauri ya madai na usuluhishi kama inavyoelekezwa kwenye sheria ya kazi na  'plea bargain' inayotumika kwenye mashauri ya jinai ambayo hayajafika mahakamani au yamefika mahakamani lakini uamuzi haujatolewa?" amesema Jaji Mfawidi hiyo na kuongeza.

...Njia hizi ziliwahi kutumika zamani kabla ya kutawaliwa na wakoloni kupata uhuru kwa lengo la kuhakikidha jamii inaishi kwa kuelewana na kuheshimiana huku ikisaidia  kurejesha umoja, amani na mtangamano katika jamii,".

Hata hivyo Jaji Mfawidhi Tiganga alionya kuwa usuluhishi huo haujumuishi mashauri ya ubakaji, ndoa za utotoni, mtoto kupewa mimba, ukeketaji na masuala mengin3 yanayofanana na hayo.

"Zipo baadhi ya jamii zetu imezoeleka wazazi kwenda kuzungumza mtu aliyefanya ukatili kwa watoto  na wanakubaliana naye wakiamini wamesuluhishwa na wanapokea fedha ambazo huziita fidia na kwa bahati mbaya  mtoto ambaye ni muathirika anakuwa hashirikishwi kwenye mazungumzo hayo," alionya Jaji Tiganga na kuongeza


.... Usuluhishi huu  haihusishi migogoro yote ya  jinai kwa sababu jamii zetu zinasuluhusiha mfano mtoto kabakwa au kaolewa kwenye umri mdogo wazazi wanapokea ambazo huziita fidia hii si sawa. Nikumbushe tu mashauri ya aina hii hayasuluhishiki,".




Jaji Tiganga amezitaja baadhi ya jamii ambazo kwa muda mrefu zimekuwa na taratibu zao za kumaliza migogoro kwa njia ya usuluhishi kuwa ni pamoja na Wamaasai na Wameru .



Mahakimu na majaji mjutahidi kutumia usuluhishi kaika migogoro inayoletwa mbele yenu 


Awali, Mkuu wa mkoa wa Arusha, John Mongela amesema kuwa muhimili wa Mahakama umebadilika sana ambapo kwa sasa hata watumishi wake wanaweza kuchangamana na watu wa kada nyingine kwenye hafla zao jambo ambalo halikuwa likitokea miaka ya nyuma.

"Mahakama hapo zamani ilikuwa vigumu sana kukuta kwaya maigizo hata watu kuchangamana kama ilivyo leo mahakama inakuwa rafiki na inakuwa kimbilio inaongeza imani sana kwa wananchi," amesema mkuu wa mkoa Mongela na kuongeza.

....Niwapongeze mahakama kanda ya Arusha kwa mura niliokuwa hapa kila siku inavyokwenda kuna ushuhuda mkubwa sana kwa huduma zinavyozidi kuboreka  inazidi kuongeza amani na utulivu kwenye mkoa na inazidi kuongeza tija kwenye shughuli za maendeleo za mkoa wetu,".

Mongela amesema kuwa kauli mbiu ya wiki ya sheria "Utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kukuza uchumi endelevu wajibu wa mahakama na wadau imewapa elimu kujua wajibu wa mahakama kwenye kuchangia maendeleo ya nchi na watu wake.

"Uongozi wa mkoa wakati wowote tutakuwa tayari kuisaidia mahakama kwa namna yoyote itakapohitajika  kwani dhana hii tunaamini itaenda kuketa mabadiliko makubwa nchini na kwenye mkoa wetu kwa kuleta utulivu na amani,".


Kwa upande wake, Wakili wa Serikali Mkuu, Vertas  Mlay amesema kuwa sheria ya usuluhishi na uwekezaji ni nyenzo muhimu katika kukua uchumi wa nchi na wa mtu mmoja mmoja.


 Jumla ya watoa huduma za usuluhishi, majadiliano na wapatanishi 498 wameshanishwa ambapo mchakato unendelea ili kupata wengine wenye sifa ili majina yao yawasilishwe kwenye baraza la kimataifa la utatuzi wa migogoro.

Wataalam hao wamepitishwa na jopo la ithibati linalowajumuisha mwanasheria mkuu wa serikali, Wakili mkuu wa serikali, Rais wa Chama Cha Mawakili Tanganyika, (TLS) taasisi ya usuluhishi nchini na wajumbe kutoka baraza la ujenzi chini ya uratibu wa wizara ya sheria na katiba. 


0 Comments:

Post a Comment