Thursday, May 5, 2022

MBIVU MBICHI RUFAA YA SABAYA KUJULIKANA KESHO

 


MBIVU mbichi  rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wanaopinga uamuzi wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka 30 kujulikana kesho Mei 6, 2022 wakati Mahakama Kuu Kanda ya Arusha inapotarajiwa kutoa uamuzi kwenye  

 

 

Jaji Sedekia Kisanya wa mahakama Kuu Kanda ya Musoma anayesikiliza rufaa hiyo namba 129/2021 kwenye mahakama Kuu Kanda ya Arusha alipanga tarehe hiyo Machi 18, mwaka  siku shauri hilo llipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

 

Katika rufaa hiyo mawakili wa waleta rufaa waliwasilisha hoja 14 ikiwemo kuwa hakimu hakufanyia tathmini ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo katika kufanya uamuzi wake na kuwa polisi hawakufanya uchunguzi wao ipasavyo.

 

 

 

Sabaya na wenzake Silvester Nyengu na Daniel Mbura wanaiomba mahakama kuwafutia hukumu na adhabu waliyopewa ya kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia silaha ambayo hakimu katika uamuzi wake kwenye shitaka moja aliwatia hatiani kwa kosa la unyang'anyi wa makundi iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi Arusha.

 

Hoja hizo ziliwasilishwa kwa kupokezana na mawakili wa mleta maombi wa kwanza Sabaya, Majura Magafu na Moses Mahuna ambapo walidai polisi hawakufanya upelelezi wao vizuri ndiyo sababu hawakuweza kubaini malalamiko ya shahidi wa sita, Bakari Msangi yalitokana na tofauti zake na Sabaya wakati akiwa UV CCM na hakupenda alipoteuliwa kuwa DC wa Hai.

 

 

 

Wakili Magafu aliieleza mahakama hiyo kuwa kwamujibu wa kifungu cha 312 cha uendeshaji mashauri ya jinai, (CPA) sheria inata jaji au hakimu anapoandika hukumu yake inabidi afanye mchanganuo wa kina juu ya ushahidi ulioletwa mbele yake asipofanya hivyo hiyo hukumu inakuwa ni batili.

 

"Kila hakimu au jaji anayo staili au utaratibu wake wa kuandika hukumu lakini kitu cha msingi anachotakiwa kuangalia ni kupitia viini vyote vya mashitaka na ushahidi kama ulivyotolewa na pande zote," ameeleza Magafu huku akirejea mashauri yaliyowahi kufanyiwa uamuzi na mahakama ya rufani na kuongeza.

 

....Mheshimiwa Jaji,  hakimu aliyesikiliza hili shauri hakufanya uchambuzi wa kina matokeo yake akatoa hukumu ambayo tunaiona haikuwa stahiki. Kama mheshimiwa hakimu angefanya uchambuzi wa kina juu ushahidi ulioletwa mbele yake angeweza kugundua mambo yafuatayo.

 

....Hati ya mashitaka iliyoletwa mbele yake haikukidhi matakwa ya kisheria ilikuwa 'defective' ushahidi uliotolewa haukuendana na hati ya mashitaka yaliyokuwa mbele yake,".

 

Magafu alidai kuwa kesi iliyofunguliwa na kuwafunga wateja wao ilikuwa ya majungu na ilisababishwa na polisi kutofanya upelelezi ipaswavyo.


"Kwa nini polisi wanatakiwa kufanya upelelezi na upelelezi uwe wa kina ili waweze kugundua kosa limefanyika au halikufanyika kama kesi ni ya majungu au si majungu katika hii kesi tunayoona hapa ilikuwa ya majungu," amedai wakili Magafu na kuongeza

 

...Pw 6 ( shahidi wa sita wa Jamhuri, Bakari Msangi) na mleta rufaa wa kwanza , (Sabaya) walikuwa wanatofautiana walipokuwa UV CCM na PW 6 hakufurahi mleta rufaa wa kwanza kuteuliwa kuwa DC hakufurahi.

 

....Polisi wangechunguza vizuri wangejua ni uongo. Pw 6 anasema alipekuliwa akaibiwa 390,000 na simu lakini PW 4 anasema alishuhudia PW 6 akipekuliwa alichoshuhudia aliona akinyang'anywa simu na wallet," .

 

"Kwenye ukurasa wa 113 ya uamuzi mahakama ilieleza kwenye hoja za majumuisho za mawakili . Mahakama ilisema kuwa shahidi wa saba na wa 11 wote wawili walisema duka hilo liko Bondeni Street karibu na Soko Kuu tunajiuliza hilo ni sawa?

 

“ Kwenye ukurasa wa 124 Gwakisa anasema kuwa alifahamishwa na mrufani wa kwanza bwana Lengai ole Sabaya kuwa aliwakamata PW2 ( Noman Jasin) na PW 4 (Hajirini Saad) kwenye duka lao huo sokoni,”. 

 

“Siku ya tarehe 12 /1 / 2021 (Gwakisa) alienda yeye PW 7 PW 2, (Josin) PW4 (Hajirin Saad Hajirini)kwenye duka la PW 2 na PW 4 lililoko bondeni street lililoko karibu na Soko Kuu. Duka linalozungumziwa hapa ni la pw 1 (Mohamed Saad lililopo bondeni street near market . Pw 7 hakuwahi kuzungumzia duka la PW 1 ambalo ndilo lipo kwenye hati ya mashitaka,"..

 

 

 

"Mheshimiwa Jaji issue sio kumiliki duka ila ni kumiliki duka eneo ambalo tukio wa unyang'anyi wa kutumia silaha umefanyika. Pw 1 (Mohamed Saad) anaonekana kuwa na maduka zaidi ya matatu.  Duka la kwanza liko bondeni street ambalo haliungwi mkono na ushahidi wowote," amedai wakili Mahuna na kuongeza. 

 

...Duka la pili ni hili lililopo mtaa wa sokoni ambalo hata yeye anasema , duka la tatu lipo Bondeni Kati kulingana na p7 (Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha, Gwakisa Minga)na duka la nne ni la TIN linasema Shaahid Store linaonekana liko nyamwezi.

 

.,Ni duka lipi linaloungwa mkono na hati ya mashitaka ni lipi?Kuna makosa kusema ushahidi wa mashahidi wa saba na wa kwanza wanashabihiana kwenye eneo kwani wametofautiana kama nilivyoeleza hapo juu,"

 

MAWAKILI WA SERIKALI WAPANGUA HOJA ZA MAWAKILI WA SABAYA

 

Mawakili wa Serikali, waliomba mahakama hiyo kutupilia mbali  hoja zote 14 za rufaa zilizowasilishwa na mawakili wa waleta rufaa kwani hazina msingi kisheria huku wakisisitiza  kuwa Sabaya kwenye ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa alifika kwenye eneo la tukio.

 

 

Pia walieleza kuwa hakimu alifanya uchambuzi wa kina wa ushahidi wa mashahidi na vielelezo na kutoa hukumu na adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na jeshi la polisi wakati wa upelelezi.

 

 

"Kwa kupitia hoja tulizowasilisha ni kuwa mahakama ya chini ilifanya 'proper evaluation' na kufanya maamuzi sahihi na mahakama ilijielekeza kuangalia ushahidi wa msingi wa rufani  wa kwanza mpaka wa tatu (Sabaya, Nyengu na Mbura) ulizingatiwa na kwa nini waliunganishwa mahakama ilitimiza wajibu wake ipasavyo hatujaona mahali popote mahakama hii itaingilia ule uamuzi," alieleza Wakili wa serikali Baraka Mgaya na kuongeza.

 

"Tunaomba mahakama yako itupilie mbali sababu zote 14 zilizowasilishwa na kuzingatia hukumu na adhabu iliyotolewa na mahakama ya chini,".

 

 

 

"Wanasema kuwa shahidi wa tatu alisema fedha alizokuwa  nazo zilikuwa kwa ajili ya kununua vitu vya nyumbani tumepitia mwenenendo hatujaona mahali amesema kuwa alienda kununua vitu vya nyumbani ,hiki ni kitu kipya," alisema wakili Mgaya na kuongeza.

 

...Wanasema shilingi 35,000 ingewezaje kununua neti lakini hili jambo linaibuliwa kwenye rufaa kwa sababu kwenye ushahidi wake kulingana na mwenendo alisema alienda kununua neti baada ya kupata mteja ambapo baada ya kuchagua neti kabla ya kwenda kulipa akawekwa chini ya ulinzi,".

 

"Hakuna sheria yoyote inayosema kuwa ukifanya PH unazuiliwa kufanya uchunguzi na ukipata ushahidi mwingine hauwezi kuutumia hiyo ni hoja dhaifu, isiitumie na hakuna mazingira kwenye kesi hii kuwa ilipikwa

"

 

Mgaya alieleza kuwa waleta rufaa wanadai ushahidi wa shahidi wa sita, Bakari Msangi usiaminiwe jambo aliloeleza kuwa katika kuangalia uaminifu wa shahidi unaangalia msimamo wa ushahidi aliutoa ukiulinganisha na ule uliotolewa na mashahidi wengine pamoja na wa mleta rufaa, Sabaya  utaona shahidi alisema kweli.

 

Aliiomba mahakama hiyo kuzingatia ushahidi wa Shahidi wa sita, Bakari kuwa hauna tofauti na shahidi wa pili, Numan Josin, shahidi wa tatu, Shahidi wa nne, Hajirin Saad Hajini, Shahidi wa tano ambaye ni mmiliki wa duka la jirani aliyesema alimuona Mleta rufani wa kwanza, Sabaya akiingia dukani kwa shahidi wa kwanza Mohamed Asaad Hajirini

 

"Mh jaji 'story' aliyotoa PW 6 (Msangi) ukiangalia mwendelezo wake hauna tofauti na PW (shahidi) wa pili, watatu na wa nne sehemu niliyokuwa naomba mahakama yako izingatie ushahidi wa watano ambaye ni mmiliki wa duka la jirani ambaye anasema alimuona mleta rufaa wa kwanza majira ya jioni akiingia dukani hapo," alisema Mgaya na kuongeza

 

...Na ushahidi wa mleta rufaa wa kwanza, (Sabaya)  ambaye anakiri siku ya tukio alikuwa Arusha na akihitaji kumu 'interrogate' PW 1 (shahidi wa kwanza, Mohamed Saad Hajirini.Hivyo ukiangalia maelezo hayo utaona PW 6 Msangi ni mkweli na hakuna sababu ya kumtilia mashaka,", 

 

 

 

"Mleta rufaa wa pili, Nyengu  utofauti wake wa kile alichokubali kwenye  usomaji wa maelezo ya awali (PH ) kuwa yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya na kile alichokuja kujitetea kwa kujikana,". 

 

" Wakati wa PH  alisema yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya baada ya ushahidi wakati akijitetea akasema yeye si msaidizi binafsi wa Sabaya.Huu ni uongo unaojaribu kujiweka mbali na mleta rufaa wa kwanza ili asionekane kuwa alikuwa kwenye tukio," alieleza Mgaya. 

 

Wakili wa serikali Mwandamizi, Veridiana Mlenza alieza mahakama hiyo kuwa sheria na taratibu zote zilizingatiwa wakati wa kuwasomea waleta rufaa hayo PH na hiyo inathibitishwa na hatua ya rufani hao na mawakili wao kusaini taarifa za warufani mara baada ya kusomwa mahakamani.

 

 

Kwa upande wake wakili wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga alieleza mahakama hiyo kuwa jambo la msingi ni kama shahidi wa sita, Msangi alifika hospitali na alifanyiwa uchunguzi na majibu ya mdomo ya shahidi wa 10  alithibitisha hiyo.

 

"Shahidi wa pili, Josin alisema kuwa kulikuwa na vurugu ndiyo sababu hakuona watu waliochukua fedha. Hiyo inajibu hoja za waleta rufaa  kuwa iweje alishindwa kumfahamu mtu waliyekaa naye dukani kwa saa tatu aje kumtambua kwa dakika moja," alieleza wakili wa serikali, Mtenga na kuongeza.  

 

"Ushahidi kuwa PW 2 alipigwa upo na kulikuwa na vurugu ila alimtambua mleta rufaa wa pili, (Silvester Nyegu) akiwa nyumbani kwa sababu alimuona kwa karibu wakati akimkabidhi simu na hili jambo halijaenda kwenye msingi wa kesi,".

 

"Pw 2 (Shahidi wa pili wa Jamhuri) wakati akipekuwa alikuwa anahojiwa na mleta rufaa wa kwanza (Sabaya) hivyo asingeweza kuona yanayoendelea kwenye kaunta na kwa maelezo yake alikuwa anahojiwa na mtu anayetisha huwezi kuwa unaangalia angalia pembeni mara kwa mara,".

 

Mtenga alieleza mahakama kuwa hoja ya kwa nini picha za CCTV hazikuletwa mahakamani hapo zinajibiwa na ushahidi wa shahidi wa saba upande wa jamhuri ambaye ni Mkuu wa upelelezi wa polisi wilayani Arusha, Gwakisa.

 

"Shahidi wa saba wa jamhuri akitoa ushahidi wake alisema kamera zilikuwa zimeingiliwa kwa maana ya kwamba kati ya sita mbili ziligeuziwa ukutani na nne zilikuwa zinaonyesha maeneo mengine,".

 

Hata hivyo , Jaji Kisanya aliingilia kati akauliza  shahidi namba moja alisema kuwa aliangalia tukio lote kwenye CCTV ila hao wengine wanasema haikutolewa  mahakamani kwa kuwa ilichezewa.

 

Wakili Mtenga alieleza mahakama kuwa suala hilo linajibiwa na ushahidi wa shahidi huyo ambaye aliieleza mahakama hiyo kuwa hakuweza kujua walichukua fedha kwani kamera mbili tu ndiyo hazikuingiliwa ambapo upande wa waleta rufaa  hawakumuuliza endapo hizo kamera mbili zikuwa zinaelekea kaunta.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment