MBIVU mbichi rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili wanaopinga uamuzi wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha kuwapa adhabu ya kifungo cha miaka 30 kujulikana kesho Mei 6, 2022 wakati Mahakama Kuu Kanda ya Arusha inapotarajiwa kutoa uamuzi kwenye
Jaji Sedekia
Kisanya wa mahakama Kuu Kanda ya Musoma anayesikiliza rufaa hiyo namba 129/2021
kwenye mahakama Kuu Kanda ya Arusha alipanga tarehe hiyo Machi 18,
mwaka siku shauri hilo llipofika mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Katika rufaa hiyo
mawakili wa waleta rufaa waliwasilisha hoja 14 ikiwemo kuwa hakimu hakufanyia
tathmini ushahidi na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo katika kufanya
uamuzi wake na kuwa polisi hawakufanya uchunguzi wao ipasavyo.
Sabaya na wenzake
Silvester Nyengu na Daniel Mbura wanaiomba mahakama kuwafutia hukumu na adhabu
waliyopewa ya kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa ya unyang'anyi wa kutumia
silaha ambayo hakimu katika uamuzi wake kwenye shitaka moja aliwatia hatiani
kwa kosa la unyang'anyi wa makundi iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi
Arusha.
Hoja hizo ziliwasilishwa
kwa kupokezana na mawakili wa mleta maombi wa kwanza Sabaya, Majura Magafu na
Moses Mahuna ambapo walidai polisi hawakufanya upelelezi wao vizuri ndiyo
sababu hawakuweza kubaini malalamiko ya shahidi wa sita, Bakari Msangi yalitokana
na tofauti zake na Sabaya wakati akiwa UV CCM na hakupenda alipoteuliwa kuwa DC
wa Hai.
Wakili Magafu aliieleza
mahakama hiyo kuwa kwamujibu wa kifungu cha 312 cha uendeshaji mashauri ya
jinai, (CPA) sheria inata jaji au hakimu anapoandika hukumu yake inabidi afanye
mchanganuo wa kina juu ya ushahidi ulioletwa mbele yake asipofanya hivyo hiyo
hukumu inakuwa ni batili.
"Kila hakimu au
jaji anayo staili au utaratibu wake wa kuandika hukumu lakini kitu cha msingi
anachotakiwa kuangalia ni kupitia viini vyote vya mashitaka na ushahidi kama
ulivyotolewa na pande zote," ameeleza Magafu huku akirejea mashauri
yaliyowahi kufanyiwa uamuzi na mahakama ya rufani na kuongeza.
....Mheshimiwa
Jaji, hakimu aliyesikiliza hili shauri hakufanya uchambuzi wa kina
matokeo yake akatoa hukumu ambayo tunaiona haikuwa stahiki. Kama mheshimiwa
hakimu angefanya uchambuzi wa kina juu ushahidi ulioletwa mbele yake angeweza
kugundua mambo yafuatayo.
....Hati ya mashitaka
iliyoletwa mbele yake haikukidhi matakwa ya kisheria ilikuwa 'defective' ushahidi
uliotolewa haukuendana na hati ya mashitaka yaliyokuwa mbele yake,".
Magafu alidai kuwa kesi
iliyofunguliwa na kuwafunga wateja wao ilikuwa ya majungu na ilisababishwa na
polisi kutofanya upelelezi ipaswavyo.
...Pw 6 ( shahidi wa
sita wa Jamhuri, Bakari Msangi) na mleta rufaa wa kwanza , (Sabaya) walikuwa
wanatofautiana walipokuwa UV CCM na PW 6 hakufurahi mleta rufaa wa kwanza
kuteuliwa kuwa DC hakufurahi.
....Polisi wangechunguza
vizuri wangejua ni uongo. Pw 6 anasema alipekuliwa akaibiwa 390,000 na simu
lakini PW 4 anasema alishuhudia PW 6 akipekuliwa alichoshuhudia aliona
akinyang'anywa simu na wallet," .
"Kwenye ukurasa wa
113 ya uamuzi mahakama ilieleza kwenye hoja za majumuisho za mawakili .
Mahakama ilisema kuwa shahidi wa saba na wa 11 wote wawili walisema duka hilo
liko Bondeni Street karibu na Soko Kuu tunajiuliza hilo ni sawa?
“ Kwenye ukurasa wa 124
Gwakisa anasema kuwa alifahamishwa na mrufani wa kwanza bwana Lengai ole Sabaya
kuwa aliwakamata PW2 ( Noman Jasin) na PW 4 (Hajirini Saad) kwenye duka lao huo
sokoni,”.
“Siku ya tarehe 12 /1 /
2021 (Gwakisa) alienda yeye PW 7 PW 2, (Josin) PW4 (Hajirin Saad Hajirini)kwenye
duka la PW 2 na PW 4 lililoko bondeni street lililoko karibu na Soko Kuu. Duka
linalozungumziwa hapa ni la pw 1 (Mohamed Saad lililopo bondeni street near
market . Pw 7 hakuwahi kuzungumzia duka la PW 1 ambalo ndilo lipo kwenye hati
ya mashitaka,"..
"Mheshimiwa Jaji
issue sio kumiliki duka ila ni kumiliki duka eneo ambalo tukio wa unyang'anyi
wa kutumia silaha umefanyika. Pw 1 (Mohamed Saad) anaonekana kuwa na maduka
zaidi ya matatu. Duka la kwanza liko bondeni street ambalo haliungwi
mkono na ushahidi wowote," amedai wakili Mahuna na kuongeza.
...Duka la pili ni hili
lililopo mtaa wa sokoni ambalo hata yeye anasema , duka la tatu lipo Bondeni
Kati kulingana na p7 (Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha, Gwakisa Minga)na duka
la nne ni la TIN linasema Shaahid Store linaonekana liko nyamwezi.
.,Ni duka lipi
linaloungwa mkono na hati ya mashitaka ni lipi?Kuna makosa kusema ushahidi wa
mashahidi wa saba na wa kwanza wanashabihiana kwenye eneo kwani wametofautiana
kama nilivyoeleza hapo juu,"
MAWAKILI WA SERIKALI
WAPANGUA HOJA ZA MAWAKILI WA SABAYA
Mawakili wa Serikali,
waliomba mahakama hiyo kutupilia mbali hoja zote 14 za rufaa
zilizowasilishwa na mawakili wa waleta rufaa kwani hazina msingi kisheria huku
wakisisitiza kuwa Sabaya kwenye ushahidi wake aliieleza mahakama kuwa
alifika kwenye eneo la tukio.
Pia walieleza kuwa
hakimu alifanya uchambuzi wa kina wa ushahidi wa mashahidi na vielelezo na
kutoa hukumu na adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria kutokana na uchunguzi
wa kina uliofanywa na jeshi la polisi wakati wa upelelezi.
"Kwa kupitia hoja
tulizowasilisha ni kuwa mahakama ya chini ilifanya 'proper evaluation' na
kufanya maamuzi sahihi na mahakama ilijielekeza kuangalia ushahidi wa msingi wa
rufani wa kwanza mpaka wa tatu (Sabaya, Nyengu na Mbura) ulizingatiwa na
kwa nini waliunganishwa mahakama ilitimiza wajibu wake ipasavyo hatujaona
mahali popote mahakama hii itaingilia ule uamuzi," alieleza Wakili wa
serikali Baraka Mgaya na kuongeza.
"Tunaomba mahakama
yako itupilie mbali sababu zote 14 zilizowasilishwa na kuzingatia hukumu na
adhabu iliyotolewa na mahakama ya chini,".
"Wanasema kuwa
shahidi wa tatu alisema fedha alizokuwa nazo zilikuwa kwa ajili ya
kununua vitu vya nyumbani tumepitia mwenenendo hatujaona mahali amesema kuwa
alienda kununua vitu vya nyumbani ,hiki ni kitu kipya," alisema wakili
Mgaya na kuongeza.
...Wanasema shilingi
35,000 ingewezaje kununua neti lakini hili jambo linaibuliwa kwenye rufaa kwa
sababu kwenye ushahidi wake kulingana na mwenendo alisema alienda kununua neti
baada ya kupata mteja ambapo baada ya kuchagua neti kabla ya kwenda kulipa
akawekwa chini ya ulinzi,".
"Hakuna sheria
yoyote inayosema kuwa ukifanya PH unazuiliwa kufanya uchunguzi na ukipata
ushahidi mwingine hauwezi kuutumia hiyo ni hoja dhaifu, isiitumie na hakuna
mazingira kwenye kesi hii kuwa ilipikwa
"
Mgaya alieleza kuwa
waleta rufaa wanadai ushahidi wa shahidi wa sita, Bakari Msangi usiaminiwe
jambo aliloeleza kuwa katika kuangalia uaminifu wa shahidi unaangalia msimamo
wa ushahidi aliutoa ukiulinganisha na ule uliotolewa na mashahidi wengine
pamoja na wa mleta rufaa, Sabaya utaona shahidi alisema kweli.
Aliiomba mahakama hiyo
kuzingatia ushahidi wa Shahidi wa sita, Bakari kuwa hauna tofauti na shahidi wa
pili, Numan Josin, shahidi wa tatu, Shahidi wa nne, Hajirin Saad Hajini,
Shahidi wa tano ambaye ni mmiliki wa duka la jirani aliyesema alimuona Mleta rufani
wa kwanza, Sabaya akiingia dukani kwa shahidi wa kwanza Mohamed Asaad Hajirini
"Mh jaji 'story'
aliyotoa PW 6 (Msangi) ukiangalia mwendelezo wake hauna tofauti na PW (shahidi)
wa pili, watatu na wa nne sehemu niliyokuwa naomba mahakama yako izingatie
ushahidi wa watano ambaye ni mmiliki wa duka la jirani ambaye anasema alimuona
mleta rufaa wa kwanza majira ya jioni akiingia dukani hapo," alisema Mgaya
na kuongeza
...Na ushahidi wa mleta
rufaa wa kwanza, (Sabaya) ambaye anakiri siku ya tukio alikuwa Arusha na
akihitaji kumu 'interrogate' PW 1 (shahidi wa kwanza, Mohamed Saad
Hajirini.Hivyo ukiangalia maelezo hayo utaona PW 6 Msangi ni mkweli na hakuna
sababu ya kumtilia mashaka,",
"Mleta rufaa wa
pili, Nyengu utofauti wake wa kile alichokubali kwenye usomaji wa
maelezo ya awali (PH ) kuwa yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya na kile
alichokuja kujitetea kwa kujikana,".
" Wakati wa
PH alisema yeye ni msaidizi binafsi wa Sabaya baada ya ushahidi wakati
akijitetea akasema yeye si msaidizi binafsi wa Sabaya.Huu ni uongo unaojaribu
kujiweka mbali na mleta rufaa wa kwanza ili asionekane kuwa alikuwa kwenye
tukio," alieleza Mgaya.
Wakili wa serikali
Mwandamizi, Veridiana Mlenza alieza mahakama hiyo kuwa sheria na taratibu zote
zilizingatiwa wakati wa kuwasomea waleta rufaa hayo PH na hiyo inathibitishwa
na hatua ya rufani hao na mawakili wao kusaini taarifa za warufani mara baada
ya kusomwa mahakamani.
Kwa upande wake wakili
wa serikali mwandamizi, Ofmed Mtenga alieleza mahakama hiyo kuwa jambo la
msingi ni kama shahidi wa sita, Msangi alifika hospitali na alifanyiwa
uchunguzi na majibu ya mdomo ya shahidi wa 10 alithibitisha hiyo.
"Shahidi wa pili,
Josin alisema kuwa kulikuwa na vurugu ndiyo sababu hakuona watu waliochukua
fedha. Hiyo inajibu hoja za waleta rufaa kuwa iweje alishindwa kumfahamu
mtu waliyekaa naye dukani kwa saa tatu aje kumtambua kwa dakika moja," alieleza
wakili wa serikali, Mtenga na kuongeza.
"Ushahidi kuwa PW 2
alipigwa upo na kulikuwa na vurugu ila alimtambua mleta rufaa wa pili,
(Silvester Nyegu) akiwa nyumbani kwa sababu alimuona kwa karibu wakati
akimkabidhi simu na hili jambo halijaenda kwenye msingi wa kesi,".
"Pw 2 (Shahidi wa
pili wa Jamhuri) wakati akipekuwa alikuwa anahojiwa na mleta rufaa wa kwanza
(Sabaya) hivyo asingeweza kuona yanayoendelea kwenye kaunta na kwa maelezo yake
alikuwa anahojiwa na mtu anayetisha huwezi kuwa unaangalia angalia pembeni mara
kwa mara,".
Mtenga alieleza mahakama
kuwa hoja ya kwa nini picha za CCTV hazikuletwa mahakamani hapo zinajibiwa na
ushahidi wa shahidi wa saba upande wa jamhuri ambaye ni Mkuu wa upelelezi wa
polisi wilayani Arusha, Gwakisa.
"Shahidi wa saba wa
jamhuri akitoa ushahidi wake alisema kamera zilikuwa zimeingiliwa kwa maana ya
kwamba kati ya sita mbili ziligeuziwa ukutani na nne zilikuwa zinaonyesha
maeneo mengine,".
Hata hivyo , Jaji Kisanya
aliingilia kati akauliza shahidi namba moja alisema kuwa aliangalia tukio
lote kwenye CCTV ila hao wengine wanasema haikutolewa mahakamani kwa kuwa
ilichezewa.
Wakili Mtenga alieleza
mahakama kuwa suala hilo linajibiwa na ushahidi wa shahidi huyo ambaye
aliieleza mahakama hiyo kuwa hakuweza kujua walichukua fedha kwani kamera mbili
tu ndiyo hazikuingiliwa ambapo upande wa waleta rufaa hawakumuuliza
endapo hizo kamera mbili zikuwa zinaelekea kaunta.

0 Comments:
Post a Comment