RAIS, Samia Suluhu Hassan, amekamilsha uzinduzi wa filamu ya Royal Tour nchini Marekani huku akiwakaribisha wageni kutoka duniani na Marekani kutembelea Tanzania.
Amekamilisha uzinduzi huo usiku wa leo April 21, 2022, nchini Marekani, sawa na alfajiri ya April 22 Tanzania, katika ukumbi mashuhuri wa Paramount Theatre jijini Los Angeles, California,
Rais Samia aliyekuwa akishangiliwa na mamia ya watu mbalimbali waliohudhuria ukumbini hapo awali alitembelea studio za Paramount ambapo filamu na vipindi mbalimbali vya TV vikubwa duniani vinarekodiwa.
Pia amepata wasaa wa kusalimiana na watu mbalimbali waliofika kushuhudia uzinduzi huo akiwemo Baba mzazi wa msanii mashuhuri duniani, Rihanna, Ronald Fenty.
Wengine waliosalimiana na Rais Samia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mauly Tours ya nchini Tanzania, Mozzah Mauly.



0 Comments:
Post a Comment