MFANYABIASHARA maarufu jijii Arusha, Pendael Joel Mollel,(47) maarufu kama Pendaa na wenzake wawili amemekishwa mahakamani wakidaiwa walimuua kwa kukusudia, Steven Jimmy Kivuyo, (43).
Wamefikishwa mahakama ya wilaya ya Arusha leo na kusomewa shitaka hilo la kuua kwa kukusudia namba 9/2022 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Devota Msofe.
Akiwasomea mashitaka hayo, Wakili wa serikali Grace Madikenya ameieleza mahakama hiyo kuwa mnamo April 18, mwaka huu, kwenye maeneo ya Burka jijini Arusha Pendael, mkazi wa Kiranyi, Deogratius Joel Mollel, (35), na Onesmo Samuel Laizer, (25) mkazi wa Kiserian wanadaiwa kumuua Kivuyo kwa kukusudia
Washitakiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo hivyo litarudi mahakamani hapo Mei 10, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.
Washitakiwa wote wamerudishwa mahabusu kwenye gereza la mkoa wa Arusha, Kisongo kwani shitaka linalowakabili halina dhamana
Soma zaidi
https://habaritanzaniagracemacha.blogspot.com/2022/04/ndugu-wa-malinzi-anayedaiwa-kuuawa-na.html


0 Comments:
Post a Comment