FILAMU ya a ‘The Royal Tour’ itaoneshwa vituo vyote vya Runinga Nchini ili wananchi waione wakati uzunduzi wa Kitaifa ukifanyika jijihi Dar es Salaam, Mei 8, 2022
Mwenyekiti wa kamati ya Kitaifa ya Rais ya Kutangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi ameyasema hayo leo wakati akitoa taarifa juu ya uzinduzi wa Filamu hiyo utakaofanyika Katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC), Jijini Arusha Aprili 28, 2022.
“Mei 8, 2022 ndiyo itakuwa siku ya kitaifa ya kuzindua filamu hiyo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNICC), Dar es Salaam baada ya kuzinduliwa nchini katika kitovu cha utalii Mkoani Arusha Aprili 28, 2022 na Zanzibar Mei 7,2022, tukio hilo litakuwa Mubashara katika Runinga zote nchini”, amesema Dkt. Hassan Abbasi.
Dkt.Abbasi amesema kuwa ni matarajio ya Serikali kuonwa na watu takribani bilioni moja duniani kote katika kipindi cha miezi michache kufuatia tayari kuanza kuoneshwa katika Majukwaa mbalimbali ikiwemo Apple TV inayowafikia watu mil.130 na Amazon Prime milioni 150 duniani kote.
Amesema filamu ya Tanzania ya ‘The Royal Tour’imeshaanza kuoneshwa katika Runinga 350 za Majimbo mbalimbali nchini Marekani inayowafikia asilimia 86 ya wamarekani wote zaidi ya mil.200.
Dkt.Abbasi amesema Tanzania ni Nchi ya 9 duniani kushiriki Programu ya Royal Tour ikiwa ni ya pili Barani Afrika na ya Kwanza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

0 Comments:
Post a Comment