MWENYEKITI wa Taifa wa Chama cha TLP, Agustino Lyatonga Mrema akiwa na Mkewe , Doreen Kimbi katika ibada ya kufunga ndoa yao katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kijiji cha Kiraracha.
Aidha, Mwenyekiti huyo amesema familia ya mke wake ilimtaka alipie mahari ya Sh4.2 milioni ambapo hadi sasa ameweza kulipa Sh1 milioni.
leo Alhamisi Machi 24, 2022 anafunga tena ndoa baada ya mke wake, Rose kufariki septemba 16, mwaka jana saa 8 mchana wakati akipatiwa tiba ya shinikizo la damu kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
![]() |
| Mrema akiwa na mkewe, marehemu Rose enzi ya uhai wake |
Mrema amesema aliwatuma wazee kwa familia ya mke wake mtarajiwa, Doreen na kutakiwa kulipa kiasi hicho cha mahari.
Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwemo Waziri wa Mambo ya Ndsni nanNaibu Waziri Mkuu na kuwa mbunge wa Moshi Vijijini kabla ya jimbo hilo kugawanywa na pia kuwa mbunge wa Vunjo aada ya jimbo hilo kugawanywa.
Aidha kwa nyakati tofauti amegombea Urais wa Tanzania, ambapo kwa mara ya kwanza mwaka 1995 aligombea kwa kupitia chama cha NCCR Mageuzi na kutoa ushindani mkali kwa mgombea wa chma tawala, Benjamini William Mkapa hali iliyokilazimu chama hicho kumtumia baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere kuzunguka nchi nzima kumnadi mgombea wao.
Mrema alikihama chama hicho na kuanzisha chama kipya cha TLP ambapo mwaka 2000 aligombea Urais kwa tiketi ya chama hicho huku mwaka 2010 akisema amechoka biashara ya jumla na kusema anarudi kwenye biashara ya rejareja ambapo aligombea ubunge wa Vunjo na kushinda
Mke wa Mrema, Doreen amesema kuwa atamrudisha mzee Mrema ujanani.
"Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivi. Katika kipindi cha uchumba nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata," amesema Doreen na kuongeza.
"Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana,".








0 Comments:
Post a Comment