WANANCHI wengi mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya
jirani ya Arusha na Manyara wamejitokeza
kwa wingi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) kumpokea
mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, Freeman Mbowe.
Aidha, mapokezi hayo yalisababisha baadhi ya
barabara kufungwa kwa muda kutokana na wingi wa watu, magari na pikipiki.
Mwenyekiti wa Chama Mhe. Freeman Mbowe akipatiwa zawadi ya Ngao na Mkuki na wazee wa Machame.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mbowe kwenda Hai
tangu atoke gerezani Machi 4, mwaka huu baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka
nchini, (DPP) kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri la ugaidi na uhujumu uchumi lililokuwa
likimkabili Mbowe na wenzake watatu.
Siku alipotoka gerezani Mbowe, amekuwa
akifanya vikao mbalimbali ambapo kikao cha kwanza ni kati yake na Rais, Samia
Suluhu Hassan ambaye alimuita Ikulu jijini Dar es Salaam na kukubaliana kufanya
siasa za kistaarabu na kujenga Taifa
Wakati wa mapokezi hayo leo shughuli
mbalimbali zilisimama kwa muda wakati msafara wa Mbowe ukitoka uwanjani wa
ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, (KIA) huku barabara ya Arusha Moshi ikipitika kwa shida
kutokana na wingi wa wtau waliojitokeza kumlaki.
Aidha msururu mrefu wa magari ulisababisha
barabara hiyo kuwa na foleni kwa muda ambapo
Mbowe wakati anaondoka uwanja wa ndege msafara wake ulikuwa ukiongozwa na mbwa
aliyekuwa ameshikiliwa na kijana mmoja.
Wananchi walikuwa wakitumia usafiri wa aina
mbalimbali ambapo wengine walitumia bodaboda, bajaji, magari hukuwengine
wakitembea kwa miguu.
Wengi wa wananchi hao walikuwa wamekusanyika
eneo la njia panda ya KIA huku Jeshi ka Polisi likiimarisha ulinzi na kuongoza
msafara huo.
Mbowe aliyekuwa kwenye gari la wazi ameonekana muda wote akiwa
na furaha huku akiwapungia wananchi na kuwashukuru kwa kusema "asanteni
kunipokea tupo pamoja" kisha msafara kuondoka kuelekea Bomang'ombe zilipo
ofisi za Chadema kisha kuelekea kijijini kwake Nshara, Machame.
0 Comments:
Post a Comment