Aidha amesema chama hicho kikishika dola kitabadilisha mfumo huo wa elimu kwa kuhakikisha lugha ya Kiingereza inakuwa lugha ya kufundishia kuanzia madarasa ya awali hadi chuo kikuu.
Mbowe ameyasema hayo leo Jumamosi Machi 19, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika viwanja vya ofisi za chama hicho zilizopo Bomang'ombe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
"Kumekuwa na ubaguzi katika elimu, iko hivi, viongozi wetu wamekuwa wakituhubiria tujifunze kiswahili ni lugha yetu ya Taifa, lakini leo kiswahili hicho kinazungumzwa kwenye shule zetu za kata, viongozi wote na watu wenye uwezo wanasomesha watoto katika shule za mfumo wa kiingereza," amesema Mbowe na kuongeza.
…Chadema tukiingia madarakani, kiingereza ni lugha ya kimataifa, lazima watoto wote wafundishwe na kiingereza kiwe sehemu ya masomo kuanzia chekechea kwa kila mtanzania, hiyo ndiyo Tanzania tunayoitaka,".
APONGEZA JESHI LA POLISI
Katika hatua nyingine, Mbowe amelishukuru Jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa namna walivyoimarisha ulinzi wakati wa mapokezi yake wilaya ya Hai.
Akizungumza na wananchi waliokuwa wamekusanyika katika ofisi ya chama hicho Bomang'ombe Wilaya ya Hai Mbowe amesema “Hii ndio Tanzania tunayoitaka” .
Kabla na baada ya Mbowe kushuka kwenye uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro, (KIA) jeshi la polisi waliimarisha ulinzi kwenye uwanja huo ikiwemo malango ya kuingia na kutoka uwanjani humo pamoja na barabarani alikopita ambapo askari walionekana kuongoza msafara huo.
Msafara huo ukitoka KIA, wafuasi wa chama hicho walitembea kwa
miguu wakilisukuma gari la Mbowe hadi Bomang'ombe zilipo ofisi za chama hicho,
huku magari yakilazimika kwenda mwendo wa pole, hali iliyosababisha shughuli za
barabara kusimama kwa muda.
“Jaribu kufikiria leo
nimepokelewa Kilimanjaro (Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro) askari polisi
walikuwepo hajapigwa mtu bomu, hajakanyagwa tunayoitaka “ amesema Mbowe
Katika mapokezi hayo Mbowe amepewa zawadi mbalimbali ikiwemo
Ng'ombe
0 Comments:
Post a Comment