EACJ YAIELEKEZA TANZANIA KUREKEBISHA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA, PATA UNDANI WA UAMUZI HUU

 


MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashariki, (EACJ) imeielekeza  serikali ya Tanzania kurekebisha sheria yake ya vyama vya siasa kwani inakiuka vifungu vya mkataba wa kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika,(EAC).

 

Uamuzi huo umetolewa leo Machi 25, 2022 na majaji watano akiongozwa na ,  Jaji Mfawidhi , Yohane Masara, Jaji Mfawidhi  Msaidizi, Audace Ngiye, na Majaji Charles Nyawello, Charles Nyachae na Richard Wejuli.

 


Shauri hilo namba 3/ 2020 lilifunguliwa mahakamani hapo na Mwenyekiti wa Taifa, CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa ACT Wazalendo  marehemu Sharif Hamad, Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo,  Zito Kabwe, Mwenyekiti wa Chama cha CHAUMA, Hashim  Rungwe, Naibu Katibu Mkuu Chadema Zanzibar,  Salum Mwalimu na Kituo cha Sheria na Haki za binadamu, (LHRC) .

 

 

"Mahakama hii ina 'declare' kuwa sheria ya vyama vya siasa inakiuka vifungu vya mkataba sehemu 6 d 72 ya Jumuiya ya Afrika. Jamhuri ya Tanzania inaamriwa kurekebisha sheria ya vyama siasa iendane na mkataba," amesema Jaji Masara akisoma uamuzi huo.

 

 

Jaji Masara anasema mahakama imefikia uamuzi huo  baada ya kupitia hoja za kisheria na mawakili wa pande zote mahakama imezingatia kama ina mamlaka ya kusikiliza na kuamua shauri hili na kama sheria tajwa imekiuka mkataba wa jumuiya na kama waleta maombi wana haki ya kufungua shauri husika.

 

"Mahakama hii ina mamlaka kamili ya kusikiliza shauri hili licha ya ukweli kuwa mleta maombi namba nne, (Sharif Hamad)  ametangulia mbele ya haki," amesema Jaji Masara akisoma uamuzi huo.

 

Aidha amerejea kesi mbalimbali ambazo mahakama hiyo imefanya uamuzi kwenye mashauri yanayofanana na hili na ambayo yapo kwenye nchi wanachama. huku akiamuru kila upande kubeba gharama za kesi.

 

Katika shauri hilo linalofuatiliwa na wengi waleta maombi waliwakilishwa mawakili John Mallya, Sheki Mfinanga na Jebra Kambole huku upande wa jamhuri ukiwasilishwa na wakili, Vivian Method.

 

Awali  katika shauri hilo waleta maombi waliiomba mahakama hii itamke kuwa sheria ya vyama vya siasa nchini Tanzania ni batili na inakiuka misingi ya kidemokrasia na mkataba wa kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika mashariki, ambao kila nchi mwanachama  analazimika kufuata ikiwemo utawala wa bora na misingi ya kidemokrasia.

 

" Sheria inaruhusu Jumuiya kusitisha uanachama wa mwanachama ambaye atakiuka utawala bora au utawala wa kidemokrasia au atakayekiuka misingi ya haki za binadamu. Ndio msingi wa kuundwa kwa Jumuiya," amesema Jaji Masara  wakati akisoma uamuzi huo.

 

Jaji Masara amevitaja vipengelea  vya kisheria vinavyolalamikiwa kwenye sheria hiyo ya vyama vya siasa kuwa ni pamoja na kifungu kinachompa mamlaka msajili wa vyama vya siasa nchini kuingilia wakati wowote mafunzo mbalimbali na shughuli za chama cha siasa.

 

"Vifungu vyote hivi vinakiuka misingi ya utawala  bora, misingi ya kidemokrasia na inakiuka   mkataba wa kuanzishwa EAC. Kifungu kinachompa mamlaka msajili ya kumsimamisha uanachama mwanachama yeyote kushiriki shughuli za kisiasa," ameeleza Jaji Masara.

 

Amesema waleta maombi wanaomba mahakama hiyo itamke kuwa sheria hiyo ni batili na mahakama hii itoe amri kuwapa kila aina ya nafuu ya kisheria.

 

"Na kwamba sheria kumpa msajili uhuru wa kuingilia mambo ya ndani ya chama cha siasa. Na kwamba msajili sio mtu huru kwa kuwa anateuliwa na mwenyekiti wa chama cha siasa," amesema na kuongeza .

 

... Mahakama hii inaona kuwa nchi wanachama wanapaswa kuheshimu mkataba pamoja na mkataba wa haki za binadamu wa Afrika.Ni jukumu la nchi wanachama kuhakikisha ustawi wa watu,kulinda demokrasi pamoja haki za binadamu.

 

.... Kwa kuwa mahakama hii ina mamlaka sasa basi mahakama inasoma swala la au sheria ya vyama vya siasa inakiuka mkataba wa EAC.Mahakama hii inaona kuwa ni lazima sheria inayotungwa kwenye nchi wanachama izingatie haki za binadamu,ni lazima sheria iwe wazi kwa watu wake wajue kipi kinakatazwa na kipi kinakubali.

 

... Ni maoni ya mahakama hii kuwa sheria hii inampa msajili nguvu kubwa dhidi ya vyama vya siasa jambo ambalo ni kinyume cha mkataba wa Jumuiya kifungu cha nne cha  sheria ya vyama vya siasa.Kifungu hiki kinahusu mafunzo ya makada wa vyama vya siasa,na sheria inataka kabla ya mafunzo lazima chama cha siasa kipeleke kwa msajili 'material' yote ya kufundishia yeye msajili ndio akubali kama hayo mafunzo ni sawa ama la

 

...Waleta maombi walilalamikia hiki kifungu  kwa kuwa kinatoa mamlaka makubwa ya msajili kupangilia nini chama kifanye.Na kiongozi wa chama cha siasa  atakayekiuka sheria hii anatenda kosa la jinai na msajili atamfungia kwa muda atakaoamua yeye msajili.

 

...Kifungu hiki kinakiuka haki ya kujieleza na haki ya kukutana kinyume cha  mkataba wa Jumuiya ya Aftika Mashariki.Kifungu hiki kinakiuka misingi ya Kidemokrasia na utawala bora kinyume cha mkataba wa Jumuiya kwa nchi wanachama

 

Jaji Masara amesema kwa upande wake mjibu maombi ambaye ni mawakili wa serikali amejibu kuwa sheria hiyo haikusudii kukiuka mikataba ya kimataifa hivyo akaomba mahakama huyo itupilie mbali ombi hili.

Amedai kuwa kifungu hicho kinalenga kufanya serikali itambue,ijue kila tukio linalofanywa na vyama vya siasa. 

 

0 Comments:

Post a Comment