Tuesday, November 23, 2021

TAMSTOA; WAMILIKI WA MAGARI HAKIKISHENI MNAWALIPA MADEREVA WENU KUPUNGUZA AJALI

 


MWENYEKITI wa wamiliki wa malori wadogo na ya kati, (TAMSTOA), Chuki Shaban amesema wamiliki wa magari wana wajibu wa kuhakikisha madereva wao wana afya njema sanjari na kuwalipa mishahara na stahiki zao kwa wakati jambo litakalosaidia kupunguza ajali za barabarani.


Ameyasema hayo leo, Novemba 23,2021 wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho ya wiki ya usalama yanayoendelea kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Chuki amesema kuwa chama chao ni  kama ngazi kati ya serikali na wafanyabiashara hao hivyo wako kwenye maonyrsho hayo kutoa elimu kwa njia ya uso kwa uso sanjari na kutoa vipeperushi kwa  wamiliki wa malori ili wawe wanavisoma mara kwa mara kwa ajili ya kujikumbusha wajibu wao kama wamiliki wa malori.
 

"Tunashiriki haya maonyesho kuwaelimisha wasafirishaji juu ya umuhimu wao katika kuzuia ajali ikiwa ni pamoja na   wao kuwalipa madera mshahara na stahiki zao kwa wakati," amesema Chuki na kuongeza.

....Kuhakikisha madereva wanasafiri wakiwa na afya njema, kuhakikisha madereva wetu tunawapeleka vyuoni kusoma ili waweze kujua kwa ufasaha juu ya masuala ya usalama barabarani,".

Hata hivyo Chuki amesema kuwa kuna tatizo la mikataba ya madereva lakini unakuta wanachama wetu ambao ni wale  wenye malori yanayosafirisha mizigo nje ya nchi ndiyo wanapata ujumbe kwa urahisi.

"Lakini wamiliki wa malori yanayofanya safari zake ndani ya nchi si wanachama wetu hivyo hatuna mamlaka nao hatuwezi kuongea nao juu ya hilo," anasema Chuki na kushauri.

...Serikali ikitoa tamko wamiliki wa malori wote wajiunge na vyama vyao vya usafirishaji itakuwa ni rahisi kukutana nao na kuwafikishia huu ujumbe nini cha kufanya kwa madereva wao,".

Maonyesho hayo ya wiki ya wiki ya usalama barabarani yamezinduliwa leo Novemba 23,2021 na Rais, Samia Suluhu Hassan ambapo kauli mbiu ni "Jali maisha yako na ya wengine barabarani".

No comments:

Post a Comment