SHIRIKA la Bima la Taifa, (NIC), limewataka Watanzania waendeshaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya maadhimisho ya wiki ya usalama 2021 ya Jali maisha yako na ya wengine barabarani ili kupunguza ajali na kuepuka ajali zisizo za lazima.
Meneja Masoko na huduma kwa wateja wa shirika hilo, Isaya Mwakifulefule ameyasema hayo leo, Novemba 23,2021 wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye banda lao la maonyesho ya wiki ya usalama barabarani yanayofanyika ndani ya uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Amesema kuwa kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo itasaidia kuhakikisha awadhuru wanaosafiri kwa vyombo vya moto, wala wasipate hasara kwa kuharibu magari yao huku akiwasisitiza wahakikishe wanakatia magari yao bima ya NIC.
Mwakifulefule amesema kuwa wao ni wadau wakubwa wa maonyesho ya wiki ya usalama barabarani na wameshiriki kupitia mwavuli wa Mamlaka ya Usimamizi wa shughuli za bima nchini, (TIRA).
No comments:
Post a Comment