KAMPUNI ya mafuta na vilainishi ya Puma Energy imesema kuwa wametoa vilainishi vipya vya vyombo vya moto vyenye ubora na viwango vinavyotoa uhakika kwenye
Hayo yamesemwa leo Novemba 23,2021 na meneja mafuta na vilainishi wa kampuni hiyo, Prosper Kasenegala wakati akiongea na jopo la waandishi wa habari waliotembelea banda lao la maonyesho ya wiki ya usalama barabarani kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Arusha.
Amesema kuwa wameshiriki maonyesho hayo katika kuunga mkono wiki ya usalama barabarani kitaifa kwa kuwa wao pia ni wadau ambapo wameshirikiana na jeshi la polisi katika kuandaa na kutoa elimu.
"Tunauza mafuta pamoja na vilainishi bidhaa ambavyo vyombo vyote vya moto vinatumia hivyo kutoshiriki ingekuwa tumejitoa ufahamu kwa moja kwa sababu tunawauzia watu vitu wanavyovitumia kupunguza ajali," amesema Kasenegala na kuongeza.
.....Tumekuja na oil zetu mpya ambazo tumeanza kuziuza huu sasa ni mwezi wa pili na zinakidhi mahitaji na viwango vya watumiaji wetu wa Tanzania ambao hao ndiyo sasa wanahimizwa kuhusu usalama wa vyombo vyao ili kupunguza ajali na kupunguza idadi ya vifo na majeruhi wanaotokana na ajali kwani watu hao ni nguvu kazi ya Taifa.
....Tuko hapa kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mafuta pamoja na vilainishi. Puma Lubricant ni bidhaa yetu mpya ambayo ina mwezi wa pili sokoni tumeileta kwa ajili ya kuwawezesha watumiaji kujua matumizi sahihi.
...Tumeleta bidhaa ambayo ni kitu sahihi kinachohitajiwa na watumiaji kwa sasa kwani inakidhi mahitaji na matakwa yote ya watumiaji,".
Kasenegala amesema kuwa kuna bidhaa nyingine ambazo pia ni kilainishi kama mafuta ya breki.
"Hivi ulishajaribu kuwaza maisha ndani ya gari bila breki? Hivyo ni bidhaa ambazo tunauza pamoja na vilainishi vya injini na tunatoa elimu namna ya kutumia vilainishi hivi kwa usahihi ili kupunguza ajali za barabarani," amesisitiza meneja vilainishi huyo kutoka kampuni ya Puma Energy na kuongeza.
..Tuna bidhaa sahihi kwa matumizi sahihi, bidhaa itakayofanya malengo sahihi yaweze kufikiwa ya kupunguza ajali zinazoweza kuepukika kwa kuwa na vyombo vya usalama vilivyo salama,".
Maonyesho hayo ya wiki ya wiki ya usalama barabarani yamezinduliwa leo Novemba 23,2021 na Rais, Samia Suluhu Hassan ambapo kauli mbiu ni "Jali maisha yako na ya wengine barabarani".
No comments:
Post a Comment