SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amesema kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni hana gari linalohudumiwa na Bunge kwa kuwa Dereva wake alistaafu.
Ndugai ametoa kauli hiyo leo Jumanne, Aprili 17 wakati anatoa ufafanuzi wa mwongozo ulioombwa April 12 , mwaka huu na Mbunge Ukonga(Chadema), Mwita Waitara kuhusu watumishi wa upinzani walioondolewa.
Spika Ndugai amekiri kuwa hawapo baada ya kumaliza muda wao wa mkataba tangu Desemba mwaka jana na akasema kwa sasa wanaendelea kutazama na watalizungumza kwani linahitaji mjadala mpana hivyo akaomba upinzani wasigomee kusoma hotuba za upinzani.
Kiongozi huyo amesema mbali na watumishi wanne wa upinzani, lakini Bunge limewafungashia virago watumishi watano wa upande wa CCM hivyo nao hawana watendaji hadi Bunge litakapoamua vinginevyo kutokana na mambo ya kiusalama.
0 Comments:
Post a Comment